JAMES MBATIA AIBUKA,SASA AMVAA RAIS MAGUFULI,ASEMA MAZITO KUHUSU SERIKALI YAKE,SOMA HAPO KUJUA
James Mbatia akizungumza na Waandishi wa habari |
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR Mageuzi,James Mbatia amesema kitendo cha Rais John Magufuli kutofuata katiba ya nchi katika kuongoza nchi,basi ajiandae kushtakiwa pindi akitoka madarakani kwa kile anachoadai jinai haifi lazima atachukuliwa
hatua ,,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hata Hivyo,Mbatia amesema hatua ya kuzolota kwa uchumi,kupungukiwa kwa watalii
kuingia nchini pamoja na wafanyabiashara kuacha kuingiza mizigo katika Bandari
ya Dar es salaam kumetokana na maamuzi anayoda
ni ya kukurupuka yanayofanywa na utawala
wa Rais Magufuli.
Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na waandishi wa
habari wakati akizungumzia maamuzi ya Kamati kuu ya chama hicho yaliyokutana mwishoni mwa wiki.
Amesema hatua ya Rais Magufuli kuendelea kutoa
matamko ya kuingilia mihimili ya Mahakama,Bunge pamoja kuviamulu vyombo vya
dola ikiwemo polisi kuchukulia hatua za
mkoni ni jambo analodai linakwenda na
kinyume na taratibu za nchi.
“Leo anavunja katiba ya nchi asimamii katiba ambayo
ni mama Tanzania,nataka nimfamishe jinai haifi na atachukuliwa hatua pindi
atapotoka madarakani,na awashuhudie viongozi wa Kenya yaliyowakuta na yeye atafikishwa kwenye mahakamani ”amesema
Mbatia
Ametolea mfano kauli aliyoitoka Februali mwaka huu
ya wakati wa maazimisho ya siku ya majaji ambayo amedai kuwa Rais Magufuli
aliwahamulu majaji kuhukumu kesi za
wahujumu uchumi na kumpatia pea shilingi trioni moja zinazotokana na kesi hizo.
“Leo Rais unavyoingilia mhimili wa mahakama na
kuvitaka kuhukumu kesi na kuwatajia fedha flani wazilete ni jambo la hatari
ambalo anaingilia mhimili wa mahakama ,na ndio maana sisi tunasema
jinai haishi na hatua itachukuliwa kwa
mabaya anayoyafanya”amesema Mbatia.
Mbatia ametolea mfano mwengine pale wakati
Rais alipokuwa akiwaapisha viongozi wa jeshi la Polisi Ikulu, ambapo amedai
kuwa Rais alitoa ruhusa ya kuchukuliwa
Rushwa pale aliposema Polisi wa usalama barabarani wachukue rushwa ya ndogo ya elfu 5000 kwa
kusema iwasaidi katika kusafisha viatu huku Mbatia akisema suala hilo
linakwenda kinyume na katiba ya nchi
Mbatia ambaye ni pia ni Mwenyekiti mwenza wa Umoja
wa vyama vinavyounda Katiba ya wananchi (UKAWA) amesema hata hatua ya Rais
Magufuli ya kupambana na ufisadi haviendani ya hali harisi kwani kashfa nyingi
za ufisadi kubwa ameziacha.
“kuhusu ufisadi ndani ya nchi kila mtu anapiga nalo
kelele suala hilo,ila hali ya halisi hakuna juhudi za makusudi za kupambana na
ufisadi kwani kashfa kubwa zote za ufisadi ameziacha ikiwemo Kashfa ya Tegeta
Escrow,Kashfa ya Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere,Richmound,kashfa
hizi ameziacha kama kweli anania ya ukweli wa kupambana na ufisadi angeanza na
hizi”amesema Mbatia.
Kiongozi huyo ambaye ni waziri Kivuli wa wizara ya
Fedha na Mipango amegusia hatua ya watalii kupungua kuingia nchini amesema imechangiwa na washauri wa Rais
magufuli au Rais mwenyewe kuhusika katika kuruhusu kodi ya watalii ambayo haina
maana.
“Leo nenda hata Kenya hakuna kodi kama hizi ,leo
Magufuli anavyosema eti bora waje watalii wachache,huku ni kuzidisha uzorotaji
wa uchumi,”amesema