KIKWETE AWAPIGA VIJEMBE WANAOISEMA VIBAYA CCM,SOMA HAPO KUJUA
DK. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) amesema, watu wamesubiri sana chama hicho kimfie kikiwa mikononi
mwake, imeshindikana, anaandika Dany Tibaso.
Ametoa kauli hiyo leo wakati
akifungua mkutano wa Kamati Kuu ya CCM na kwamba, amefanya mambo mengi katika
uongozi wake wa miaka 10.
“Wale
wote ambao walidhani kuwa chama kitakufa, hakijafa na wala kuteteleka,” amesema
Dk. Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na kuongeza;
“Wapo
watu ambao walidhani kuwa chama kitakufa na wakadhani watajitokeza, lakini
chama hakijafa wala hata wao hawajatokeza.”
Dk.
Kikwete amesema kuwa kikao cha leo ndio kikao chake cha mwisho kwa kuwa atakaa
pembeni na kumkabidhi chama
mwenyekiti mpya ambaye ni Dk. John Magufuli, Rais
wa Tanzania.
Amesema,
katika kipindi chake cha uongozi ndani ya chama kwa kushirikiana na Kamati Kuu,
wameweza kufanya vyema na kukifanya chama kusonga mbele.
“Nimefanya
kazi kwa ushirikiano mkubwa na Kamati Kuu na chama kimesonga mbele,” amesema
Dk. Kikwete.
Mbwembwe nje ya ukumbi
Wakati
Rais Magufuli akiingia katika viwanja vya CCM, alishuka kwenye gari huku akiwa
na msafara mkubwa wenye ulinzi mkali.
Aliposhuka
katika gari, alikwenda moja kwa moja kwa baadhi ya wanaCCM kwa kuwasalimia huku
makada hao wakiwa wanaimba nyimbo mbalimbali za kumsifu mbalimbali ikiwa ni
pamoja na ‘Daktari wa Majipu’, ‘Bavicha hawatuwezi’.
Maandalizi ya Ukumbi
Dk.
Kikwete alitembelea ukumbi wa mikutano kwa maana ya kutaka kujiridhisha kama
maandalizi yamekamilika.
Wakati
akikagua ukumbi huo wa mikutano wa unaomilikiwa na CCM, aliwataka waandaaji
kuhakikisha watu ambao watakuwa katika ukumbi huo, wapangwe katika maeneo ambayo
hayatawasababishia usumbufu.
Mbali
na hilo, aliwataka kuhakikisha wanaweka utaratibu ambao utawawezesha watu ambao
watakuwa katika ukumbi huo kuwa katika hali ya utulivu huku akisema “mwenyekiti
anatakiwa kuandaliwa sehemu nzuri ya kukaa ambayo itamwezesha kuona watu wote.”
Ole-Sendeka alonga
Christopher
ole Sendeka, msemaji wa CCM amesema, mwenyekiti mpya atakayechaguliwa ndiye
atakaye panga kuwepo kwa misafara au mikutano kwa ajili ya kuwashukuru
wanachama.
“
Kwa sasa hatuna ratiba yoyote ya kufanya ziara katika mikoa kwa ajili ya kutoa
shukrani, tunasubiri mwenyekiti mpya atakayepatinana ndiye atakayetoa ratiba
kama kutakuwepo na kikutano ya kuwashukuru wanachama wa CCM au la” amesema ole
Sendeka.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline