CHADEMA YAJIPANGA KIMAPAMBANO 2020,DK MASHINJI APAMBANUA MIPANGO YA CHAMA,SOMA HAPO KUJUA
Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza mkakati wa kushinda Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, anaandika Pendo Omary.
Akizungumza wakati wa kufunga
kikao cha Kamati Tendaji ya Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), kilichomalizika
leo jijini Dar es Salaam Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa chama hicho
amesema, ifikapo mwaka 2018 chaguzi zote ndani ya chama zinapaswa kuwa zimekamilika
ili kujipanga na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
“Ili
tuweze kushinda ni lazima kutambua na kuhamasisha watu makini wenye sifa
stahili za kushika nafasi mbalimbali za uongozi na pia kujiunga na chama (kwa
wasio wanachama ).
“Lazima
mtambue mapema ukubwa wa kazi hii na kuanza kujipanga kuikamilisha kwa ufanisi;
hili ndilo jukumu la kwanza ninalotoa kwa baraza la vijana,” amesema
Dk. Mashinji.
Mashinji
amesema, baraza hilo linapaswa kutambua uongozi katika ngazi ya vitongoji,
vijiji na mitaa ni jukumu la vijana katika kujenga uzoefu na uelewa wa
kiuongozi ndani ya taifa.
“Katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, tunatarajia kuwa na Uchaguzi Mkuu wa madiwani,
wabunge na rais kwa bara. Kwa Zanzibar kutakuwa pia na uchaguzi wa wawakilishi
na rais wa Zanzibar.
“Kama
maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu kwa mwaka 2016, kila ngazi lazima itambue
nafasi ambazo zitagombewa kwenye eneo lake kwenye uchaguzi mkuu.
“Kwa
kuwa vijana watakuwa wameshikilia uongozi wa serikali za mitaa, hivyo ni amani
yangu kuwa nguvu kubwa itakwenda kwenye kushinda nafasi ya udiwani; hili ni
jukumu la tatu na la mwisho ninalowatuma kwa kipindi hiki,” amesema Dk.
Mashinji.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi Oline