BUNDI LA MSIBA KWA WASANII TENA,MSANII HUYO AFARIKI DUNIA,SOMA HAPO KUJUA
Msanii maarufu wa Vichekesho (Komedi)
kutoka kundi la Vituko Show Ndugu. Ismail Issa Makombe a.k.a KUNDAMBANDA,
amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Kundambanda alikuwa mgombea ubunge wa CUF na UKAWA
kwenye jimbo la Masasi - Mtwara katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Disemba
2015 baada ya ule wa Oktoba kutofanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea
wa awali wa UKAWA, Mhe. Emmanuel Makaidi (NLD).
Katika uchaguzi huo wa Disemba 2015 Kundambanda
alipata kura 14,069 dhidi ya kura 16,597 za (mshindi) Rashid Chua Chua kutoka
CCM. Taratibu za mazishi zinafanyikia nyumbani kwao Masas