UMOJA WA WAJANE WAKEMEA VITENDO VYA UNYANYASAJI...WAOMBA MSAADA KWA TAASISI ZINGINE KUUNGA MKONO
Umoja wa Wajane Tanzania (TAWIA) umesheherekea siku ya wajane duniani kwa kukemea
vikali tabia za kinyanyasaji ikiwemo kunyang’anywa mali,watoto na hata
kuhusishwa na vifo vya waume zao, vitendo vinavyofanywa na ndugu wa familia
mara tu baada ya tukio la kufariki kwa wenzi wao.
Akizungumza katika viwanja vya Mnazi mmoja, Mkurugenzi wa TAWIA, Rose Sarwat amesema
wajane wamekuwa wakipita katika wakati mgumu, na kwamba ili kukabiliana na
vitendo hivyo wanaomba Taasisis zingine kuunga mkono jitihada wanazofanya
ikiwamo kuwajengea uwezo wajane.
Amesema kwa sasa umoja wao una wajane wapatao 700 na wagane 20 amabao
wanahitaji msaada ili kuondokana na changamoto wanazopitia.
“Wajane tuna changamoto nyingi, tunafukuzwa katika nyumba tulizojenga na
wenzi wetu na wengi wetu hatui tukatolee wapi kilio chetu, tunaomba watu
wafahamu kuwa mjane anahaki sawa kama wengine…kitendo cha kumnyanyasa ni
kuharibu ndoto za watoto wake alioachiwa na mwezie.” Alisema
Katika hatua nyingine Mkurugenzi amesema TAWIA imejipanga kuanzisha kituo
cha pamoja ambacho kitasaidia wajane kupata huduma z ushauri nasaha, msaada wa
kisheria, uchumi na matibabu, lengo likiwa ni kupunguza kero wanazokutana nazo.
Hayo ni maadhimisho ya pili toka kuanzishwa kwa umoja huo hapa nchini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni