TRA YAHIMIZA WANANCHI KUTOA KODI,YATOA DARASA TOSHA CHUO CHA IFM,SOM HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imesema maendeleo
mazuri watanzania wanayoshudia katika
nchi zilizoendelea yametokana na wananchi katika nchi hizo kuwa na bidii katika kutoa kodi,
Hivyo,Mamlaka hiyo imewasihi watanzania kuwa
wazalendo na kutoa kodi kwa bidii ili
waweze kuliunua Taifa kimaendeleo.
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa (TRA) Richard Kayombo wakati wa ufunguzi wa Klabu ya Wanafunzi mamlaka hiyo katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
Kayombo amesema kwa sasa Taifa la Tanzania ili
litoke hapa lililo linaitajiaka juhudi kubwa kwa watanzania kutoa kodi kwa
bidii ili serikali iweze kutumia kodi hiyo katika kuleta maendeleo mbali mbali.
Amesema Kodi ndio njia ya msingi ambayo itaweze
kuondoa malalamiko yanatolewa kutoka kwa wananchi ikiwemo kukosa huduma muhimu
kama hospitali pamoja na barabara.
Kayombo ametolea mfano hata ujenzi wa Barabara ya
mabasi yaendeyo kasi yametokana na serikali kukopa fedha kwenye taasisi ya kimataifa
kwa kutugemea kurejesha fedha hizo kwa mapato yatakanayo na makusanyo ya kodi.
Hata Hivyo,Kayombo amewataka wanafunzi wa IFM kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza
jamii wanazotoka katika kuhimiza kutoa kodi ili maendeleo ya serikali yafikiwe
kwa wakati.
Kwa Upande wake Makamu mkuu wa Serikali ya wanafunzi
wa Chuo cha IFM,Felician Mussa ameishukuru Mamlaka hiyo kwa hatua waliyofanya
katika kufungua Klabu hizo Chuoni hapo
huku akisema wanafunzi wenzake watakuwa Mabalozi wazuri katika kuhimiza jamii
katika ukusanyaji wa kodi.
Mkurugenzi
wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na
wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika ufunguzi wa
Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi Vyuoni jijini Dar es Salaam leo.
Makamu
wa jumuiya wa wanafunzi wa Kodi katika chuo cha usimamizi wa fedha
(IFM), Amos Ojode akizungumza na kuwashukuru wafanyakazi wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania(TRA) kwa kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cho kujifunza
na kuzindua jumuiya ya wafunzi wa kaodi vyuoni katika chuo chao.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakiwa katika
uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi katika chuo cha usimamizi wa
fedha (IFM) jijin Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na
wanafuzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam leo
wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni.
Baadhi
ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) wakiwa katika
uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi katika chuo chao jijini Dar es
Salaam leo.
Meneja Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana masala akizungumza
na wanafuzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam
leo wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni.
Waziri wa Chuo
cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akizungumza na kuwashukuru wafanyakazi wa
TRA kwa kuzindua Jumuiya ya wanafunzi wa kodi jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), Elius Mbogo akizungumza
na kuwashukuru wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa
kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cho kujifunza na kuzindua jumuiya ya
wafunzi wa kaodi vyuoni katika chuo chao.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni