SHEIKH JALALA AWAKUTANISHA MASHEIKH, MAIMAMU WA MADHEHEBU TOFAUTI, WAJADILI DHULMA DHIDI YA WAPALESTINA
Masheikh na Maimamu wakiwa katika semina maalum inayohusu kutafakari juu ya kadhia ya Palestina, semina hiyo ilifanyika katika Msikiti wa Al Qadir Kigogo Post Daresalaam. |
Kiongozi
Mkuu wa Waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
amesema kila mwanadamu anawajibu kupiga vita dhidi ya matendo ya dhulma
wanayofanyiwa Wapalestina.
Hayo
ameyasema jana katika semina maalum ya Quds, iliyowakutanisha Viongozi wa Dini,
mbalimbali wakiwamo Maimam,Masheikh na Maustadhi,kutoka Madhehebu mbalimbali ya
Kiislam, semina iliyofanyika Masjid Ghadir,Kigogo Post Dar es salaam.
Katika
simina hiyo ya siku moja iliyokuwa na dhamira ya kujadili umuhimu wa kadhia ya
Palestina na jinsi inavyotuunganisha waislamu kama kadhia mama, Jalala ametumia
nafasi hiyo kufikisha ujumbe kwa umma kuwa kuna haja ya Waislamu kupinga
matendo wanayofanyiwa wapalestina kwani suala hilo halina mahusiano na uarabu
na Siasa.
Amesema wapalestina wanafanyiwa uvamizi katika
nchi yao, wamekuwa hawana Amani kama Nchi zingine na kwamba jambo hilo halikubaliki
ni lazima lipigiwe kelele ili Wapalestina waweze kupata haki zao za msingi.
“Sisi
kama waislam tumeelekezwa juu ya kujali mambo ya Waislamu wenzetu, lakini
nataka niseme wanaopata tabu pale Palestina si Waislamu peke yao, kuna Wakristo
pia niwaombe Watanzania kwa ujumla kufahamu hilo na kuwaombea wenzetu wawe na Amani”Alisema
Sheikh Jalala
Amesema
pindi Sauti inapopazwa ndivyo vyombo vya umoja wa mataifa ukavyodhi kuelelewa
ukubwa wa Tatizo na hivyo kuweza kutoa shuruhisho muhimu kwa mustakabali wa Amani
ya Palestina
“Tunaomba
vyombo vya umoja wa mataifa, Watanzania Waislamu na wasio Waislamu kuunga mkono
jitihada za kupinga dhulma dhidi ya watu wa Palestina, kwa kuwaombea ili nao
waweze kufaidi keki ya Amani kama Watanzania wanavyofanya.
Aidha
amesema Wapalestina wakristo na waislam wakae vizuri na dini zingine kama kama
ilivyo Tanzania, na hilo linawezekana kama dunia itaamua kupiga kelele juu ya
umuhimu wa Wapalestina kupewa haki zao
“Tungependa Palestina tuione ina Amani kama Tanzania,
Nchi hii inajulikana kwamba ni kisiwa cha amani, ni mahala pa maelewano, katika
historia yake ya Tanzania haitambui ubaguzi na hivyohivyo palestina iwe ni
mahala pa amani, iwe ni mahala hapana ubaguzi, watu wote wakae pamoja, wakae
kwa maelewano, dhulma isambaratike, dhulma iondoke” Alisema Jalala
Alisema unapoingalia historia ya palestina na yanayojiri katika ardhi ya
palestina ni dhulma unyonyaji,
ukandamizaji ambao ni makosa na wala hauruhusiwi kuunyamazia kimya si kwa Waislamu au Wasiokuwa Waislamu
Waislamu na Wasio Waislamu wanaikukumbuka na kuadhimisha siku ya Quds Duniani ambayo kwa maana nyingine wanaadhimisha
na kuikumbuka palestina (Msikiti mtukufu wa Quds na ardhi tukufu),
Kuikumbuka palestina na siku ya Quds ni jambo ambalola kitabia(kiakhlaq), pili ni jambo la kidini na tatu ni jambo la kiuwanaadam.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni