LHRC YAONGEZWA NGUVU, YAPEWA DOLA ZAIDI YA 2 MIL....BALOZI WA NORWAY ASIFU JITIHADA ZAO
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Kijjo Bisimba akifafanua jambo kwa waandishi wa habari. |
Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Anne-Marie Kaarstad akitia saini kuashiria makubaliano ya ufadhili huo. |
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia zoezi la utiliaji saini wa mkataba huo utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka 2016 hadi 2018. |
Kituo cha sharia
na haki za binadamu LHRC kimepata nguvu mpya ya kuendeleza mapambano ya haki za
binadamu hapa nchini baada ya kufanikiwa kupata msaada wa Krone 17Mil sawa na
dola Mil. 2.125 katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2018 kwa ajiri ya uendeshaji
wa miradi mbalimbali ya kituo hicho
Akizungumza na
Waandishi wa habari mara baada ya kutiliana saini Makao Makuu ya Kituo hicho,
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Bi Kijjo Bisimba amesema Msaada huo umekuja
wakati muafaka kwani bado kuna kazi kubwa ya kufanya ikiwamo kupigania uwepo
katiba mpya na inayokubaliwa na wananchi wote.
Amesema katika
kipindi hiki cha awamu ya Tano, kuna changamoto nyingi zinaanza kujitokeza
lakini wamejipanga kuhakikisha wanatetea na kupigania haki za binadamu katika
ardhi ya Tanzania na kwamba msaada huo utasaidia kuongeza ari kwa wafanyakazi
wa kituo hicho.
Akizungumzia
watu walionufaika na uwepo wa Kituo hicho toka kuanzishwa kwake, Bisimba
amesema tayari ya wananchi 150,000 wameweza kufikiwa na kusaidiwa katika
changamoto zao, hivyo ujio wa msaada huo utaongeza ufanisi wa kazi.
“Si mara ya
kwanza Serikali ya Norway kusaidia Kituo chetu cha sharia na haki za binadamu,
toka mwaka 2004 wamekuwa bega kwa bega na sisi, hawajatuacha gizani. Kwa kweli
tunawashukuru sana kwa kutuamini na kuendelea kutupa nguvu ya kupambania haki
za watu hapa Tanzania”Alisema Kijo Bisimba.
Kwa upande wake
Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Anne-Marie Kaarstad amesifu jitihada
zinazofanywa na Kituo cha sheria za kuhakikisha mapambano ya haki za binadamu
yanaendelea bila woga, na kwamba Nchi yake imefurahisishwa na jinsi
wanavyofanya kazi.
Amesema kufuatia
hali hiyo, Nchi ya Norway imeamua kuendelea kufanya kazi na Kituo hicho kwa
kufadhili shughuli zake, kwani wanaamini kupitia kituo hicho wananchi wengi
wananufaika ikiwamo kupata haki zao walizodhulumiwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni