MSANII NISHA AWAKUMBUKA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU KATIKA MWENZI MTUKUFU,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Msanii wa Firamu Salma Jabu maarufu Nisha akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam |
MSANII wa kike anaetamba na Filamu yake ya Kiboko Kabisa Salma Jabu maarufu Nisha ameandaa futari maalum kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.Anaandika KAROLI VISENT endelea nayo
Huku akieleza kuwa yeye kama kioo cha jamii ni wajibu wake kurudisha kwa jamii katika kile anachokipata, pia kwa mujibu wa Imani yake ya Dini ya Kiislamu hana budi kusaidia hasav kwa watoto yatima
Msanii huyo wenye kipaji cha aina yake ameyasema hay oleo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amewataka wadau wa maendeleo kuachana na kasumba ya kuwasaidia watoto au watu wenye mahitaji maalum siku za Ramadhani au sikukuu mbalimbali za Dini kwani wanahitaji msaada wa karibu zaidi na sio wa msimu kwa msimu.
Nisha ambaye ni balozi wa watoto na
msimamizi mkuu wa kituo cha Watoto Yatima cha New Hope Family kilichopo Kibada
Mwasonga Dar es Salaam amesema Futari
hiyo kwa watoto waishio mazingira magumu inataraji kufanyika siku ya Jumapili
June 26 katika shule ya Sekondari Azania ,
Amesema katika Futari hiyo inatarajiwa
kuhudhuriwa na wageni rasmi akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu, Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Paul Makonda na watu mashughuli mbalimbali,
Aidha Nisha ameeleza kuwa mashabiki wake wakae
mkao wa kula kwa filamu yake itakayo kuwa na maudhui ya watoto wanaoishi katika
mazingira magumu ambapo ametaja msanii wa Vichekesho Joti kuwa mmoja wa
wshiriki katika filamu yake hiyo ambayo imeendaliwa na kampuni yake ya Nisha
Film Production.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni