Zinazobamba

KIGOGO WA CCM AWAANGUKIA WABUNGE WA UKAWA,NI KUHUSU KUTOKA BUNGENI,SOMA HAPO KUJUA

 

Philip-Mangula

Makamu Mwenyeketi wa CCM Taifa (Bara), Philip Mangula amewaangukia wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani  na kuwaomba warudi bungeni, kwani michango yao inaumuhimu mkubwa hasa katika  Bunge la Bajeti.

Mangula ametoa kauli hiyo baada ya hatua ya wabunge wa Ukawa kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson ikiwa ni  kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani naye.Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mangula alisema michango ya wapinzani ina umuhimu mkubwa na pia ni wachangiaji wazuri bungeni.

“Michango ya wabunge wa upinzani ina umuhimu mkubwa hasa katika mijadala ya kupitisha bajeti ya nchi ambayo pia inagusa katika majimbo yao”.

“Kutoka ndani ya Bunge si njia ya kutatua tatizo kwa kuwa ndani ya vikao hivyo ndipo zinapojadiliwa changamoto za majimbo yao ambayo yote yanatemegea Bajeti Kuu” alisema Mangula.

Alisema suala la kususia vikao na kwenda kuijadili bajeti nje ya Bunge hakutaweza kuleta manufaa kwa taifa na hata kwenye majimbo yao.

Akizungumzia suala la adhabu walizopewa wabunge saba  wa upinzani, Mangula alisema kila jambo lina utaratibu na kanuni zake za kufuata.


Hakuna maoni