MAHAKAMA YAMGOMEA MBOWE TENA,SOMA HAPO KUJUA
KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba
mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali, anaandika Moses Mseti.
Mbowe alifungua kesi hiyo namba
79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni Jeshi la Polisi kupiga
marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali ya usalama nchini si
salama.
Mbowe
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo, aliwashtaki
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa madai
wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
Mbowe
ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya oparesheni
iliopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la kuishtaki serikali
kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata katiba ya nchi.
Hata
hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi ya madai
katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, akiiomba kutengua zuio hilo la
polisi.
Mohammed
Gwae, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, leo amepitia ombi
lililopelekwa mahakamani hapo na upande wa mlalamikaji anayewakilishwa na
mawakili John Mallya na Gasper Mwanalelya na kutoa uamzi.
Jaji
Gwae akitoa uamuzi wa ombi la walalamikaji amedai kuwa, amefikia hatua hiyo
baada ya walalamikaji kukosea kifungu cha kupeleka shauri hilo kortini kitendo
kilichosababisha kulitupilia mbali.
Amesema
kuwa, walalamikaji baada ya kupeleka ombi hilo kortini, upande wa wajibu maombi
unaoongozwa na mawakili, Seth Mkemwa na Robert Kidando waliweka pingamizi
wakiomba mahakama kutokusikiliza ombi hilo.
Jaji
Gwae amesema kuwa, walalamikaji katika ombi lao walikosea kutumia kanuni ya
tano kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya mwaka 2014 badala ya kanuni ya tano
kifungu kidogo cha pili ambacho kilitakiwa kutumiwa.
“Waleta
maombi wametumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu badala ya kutumia
kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili kilichotakiwa kuwepo katika kuleta ombi
na kama kifungu hiki hakijatumika hapo na ombi halipaswi kupokelewa,” amesema
Jaji Gwae.
Hata
hivyo Jaji Gwae amesema, licha ya kuwekewa pingamizi na wajibu maombi,
walalamikaji wamesema kanuni na kifungu hicho ndivyo vilitakiwa kuwepo na hivyo
vinavyopaswa kuwekwa sio sahihi.
Amesema
kuwa, katika shauri la namna hiyo, kanuni na vifungu vilivyotakiwa kuwepo ni
kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili na kanuni ya tano na kifungu kidogo cha
vya sheria ya mwaka 2014 na kwamba wao waliviweka katika maelezo (Statements)
badala ya (chember samers).
Mallya,
mwanasheria wa mpeleka maombi amesema kuwa, baada ya kukosea kanuni na vifungu
hivyo, watapeleka kwa mara nyingine ombi na kulifanyia marekebisho kama Jaji
Mohamed Gwae alivyoelekeza.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni