Pichani ni Msanii Nisha akizungumza na Waandishi habari juu ya Futari aliyowaandalia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Picha kwahisani ya Mtembezi.com.
Pichani ni watu mbali mbali wakijumuika wakati kupata futari iliyoaandaliwa na msanii huyo
Msanii wa Filamu mahiri ya “Kiboko
Kabisa’ Salma Jabu maarufu kama (Nisha) amekuwa miongoni mwa watu mashuhuri
waliojitolea kuwafuturisha watoto waishio katika mazingira magumu huku wengine
wakitokea kituo cha Watoto Yatima cha New Hope Family kilichopo Kibada
Mwasonga Dar es Salaam ambacho yeye ni msimamizi.
Watoto hao ambao walihudhuria mualiko wa futari viwanja vya
shule ya Azania jijini Dar es Salaam walifikia hatua ya kumtoa machozi msanii
huyo kutokana na dua mbalimbali walizokuwa wakisoma kuonekana kumgusa msanii
huyo, ambapo amewataka wadau mbalimbali kuunga mkono jitihadfa hizo na ziwe
endelevu ili kuwasaidia watoto hao kwani wanahitaji msaada wa karibu zaidi kama
watu wengine.
Kwa upande wa watoto hao wametoa pongezi kwa Nisha huku
wakimuombea Dua aendelee kuwaunga mkono kwa hali na mali, pia futari hiyo
ilihudhuriwa na watu wengi mashuhuri akiwemo Eshe Buheti msanii wa Filamu,
Jackline Wolper, Jini Kabula, Halima Yahya, Frola Mvungi, Snura Mushi, JK
Comedian Rajai Ayoub mshindi wa kwanza wamashindano ya Qur-an Afrika na
wasita kidunia na wengine wengi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni