MAWIO WAFUTIWA MASHTAKA MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es
Salaam leo imewafutia mashitaka mawili Siomon Mkina, Mhariri wa Mawio na Jabir
Idrisa, mwandishi wa gazeti hilo na Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, anaandika Faki Sosi.
Ni katika kesi ya uchochezi
iliyofunguliwa na serikali dhidi ya watu hao pamoja na mchapishaji wa gazeti la
Mawio, Ismail Mahboob wa Kampuni ya Flint Graphics.
Mashitaka
yaliyofutwa ni shtaka namba moja na shtaka namba tano ambapo pande zote mbili
(utetezi na mashtaka) zimeridhia kufutwa kwa mashtaka hayo mbele ya Hakimu
Thomas Simba.
Mashtaka
hayo ni kupanga njama za kufanya chapisho la uchochezi na kosa la pili ni
kuwatisha wananchi wa Zanzibar kwamba, machafuko yanawaweza kutokea Zanzibar.
Awali,
Poul Kadushi, Wakili wa Serikali aliiomba mahakama hiyo kuondoa shtaka namba
moja na tano kutokana na kukosekana kwa idhini ya Mamlaka ya Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP).
Peter
Kibatala, Wakili wa Upande wa Washitakiwa amesema kuwa, Wakili wa Serikali
amefanya busara kukubaliana na upande huo kuwa, mashtaka hayo yalikuwa na
upungufu kisheria.
Hakimu
Simba amefuta mashtaka hayo baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na
kwamba, watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matatu pekee.
Shitaka
la pili la kuchapisha chapisho la uchochezi linawakabili Idrisa mshitakiwa
namba moja, Mkina ambaye ni mshitakiwa namba mbili na Lissu, mshitakiwa namba
nne.
Shitaka
la tatu la kuchapisha magazeti bila ya kuwa na hati ya kiapo kutoka kwa msajili
wa magazeti linamuhusu Mahboob, mshitakiwa namba tatu.
Shtaka
namba nne la kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar ya kutopiga kura kwa kuhofia
umwagikaji wa damu.
Hata
hivyo, Kadushi amejibu hoja zilizowasilishwa mahakamani hapo na upende wa
utetezi kuwa, zina kasoro.
Kadushi
amedai kuwa mashitaka yote yaliyobaki katika shauri hilo yameanishwa
kwa kila kosa na kifungu chake na maelezo ya kosa hilo.
Amedai
kuwa, kifungu namba 32 (a), (b), na (c) cha makosa ya jinai kimeanisha kuwa, na
nia ya kutenda kosa ni kosa na kutenda kosa ni kosa.
Peter
Kibatala amedai kuwa, bado hoja za Kadushi hazina mashiko na kwamba, mashtaka
hayo ya matatu yaliyobaki hayana mashiko kutokana na kwamba, Sheria ya
magazeti haifanyi kazi Zanzibar na kuwa chapisho hilo lingeleta athari Zanzibar
na sio Tanzania Bara ambapo yupo waziri husika.
Kibatara
amewasilisha hoja ya kufutwa kwa mashtaka yaliyobaki kwa madai kuwa, hayana
mashiko kwa mujibu wa kifungu 31(a)(b) na (c) cha sheria ya magazeti
ambayo inampa haki raia kuikosoa serikali.
Kesi
hiyo itatajwa tena 11 Julai mwaka huu ambapo hakimu atatoa maamuzi ya kufutwa
ama kutofutwa kwa shauri hilo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni