TUNDU LISSU AILIPUA SERIKALI,ATANGAZA KUPAMBANA NAYO,SOMA HAPO KUJUA
Simon Mkina, aliyekua Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mawio (Wakwanza),na Tundu Lissu, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wakizungumza na wanahabari baada ya kutoka Mahakamani |
TUNDU Lissu, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya
Upinzani ameseme kuwa, vitendo vinavyofanywa na serikali ya sasa ni vya hovyo, anaandika Faki Sosi.
Lissu ambaye ni Mwanasheria
Mkuu wa Chadema pia Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki amesema hayo leo muda
mfupi baada ya kumaliza kusikiliza shauri lake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Kwenye
shitaka hilo, Lissu pamoja na washitakiwa wengine watatu wanadaiwa kufanya
makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchochezi kupitia gazeti la Mawio la
tarehe 14 Januari 2016.
Kwenye
gazeti hilo lililoandikwa kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’ Lissu
alinukuliwa kama mchangiaji wa gazeti hilo ambapo tayari limefutwa na serikali.
Nje
ya mahakamani hiyo Lissu amesema “nchi yetu imeingia katika giza nene, huyu
dikteta uchwara, naomba nirudie tena, huyu dikteta uchwara anahitaji kupingwa
na kila mwananchi.
“Kila
msema kweli wa nchi hii. Huu ni wakati wa kujitokeza na kusema hii ni nchi ya
vyama vingi, hii ni nchi inayotambua haki za binadamu kwenye Katiba yake.
“Hatuwezi
tukakubali nchi iongozwe kwa kauli za mdomo za mtu mmoja hata kama amechaguliwa
kuwa rais,”
Akizungumzia
kesi iliyofunguliwa na kuhusishwa kwake Lissu amesema, kesi iliyofunguliwa
na serikali dhidi yake na wahariri wa gazeti la Mawio ya uchochezi, ni
ushahidi tosha kuwa nchi imeingia kwenye giza nene la udekikteta.
Amesema,
hata sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ipo wazi kwamba, kuikosoa
serikali sio uchochezi.
“Mashtaka
haya yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezo, sio ya uchichozi hata kidogo.
Nilichosema, niliulizwa na waandishi … niliosema uchaguzi wa marudio ya
uchaguzi Zanzibar yanaweza kuviingiza visiwani hivyo kwenye machafuko na
umwagaji damu… ni kauli ya raia anayefahamu na hapendezwi na mwenendo wa
serikali” amesema Lissu.
Amesema kuwa, hata sheria ya magazeti inasema kuwa
kitetendo chochote chenye lengo la kueleza ubovu wa serikali au mamlaka yake
sio kosa.
“Nilichosema
mimi kuwa serikali hii na matendo yaki ni ya hovyo… huyo dikitekta uchwara
anahitaji kupingwa na kila mwananchi,” amesema.
“Kama
wanafikiria watatutisha kwa kutuleta mahakamani, tutamkabili mahakamani na
tutamkabili nje.
“Ni
wakati wa wazalendo kusema kuwa, Tanzania ni nchi ya vyama vingi na ina Katiba
na sheria. Katiba yetu inatambua haki za binaadamu na moja haki za binaadamu ni
kueleza ujinga wa watawala wanapofanya ujinga,” amesema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni