MRITHI WA MAKONDA KINONDONI AJITOSA KWENYE VITA YA SHAMBA LA SUMAYE,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akizungumza na wakazi wa Mwabepande alipokwenda kuwasikiliza ili kutafuta ufumbuzi juu ya mgogo wa shamba kati yao na Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye
MKUU wa Wilaya ya
Kinondoni,Ally Hapi amewahidi wananchi
wa Mabwepande wilayani humo kuwa ataumaliza mgogoro wa ardhi uliopo kati ya Waziri mkuu mstaafu,Fredrick
Sumaye na wananchi hao.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo
Hapi ametoa ahadi hiyo
leo Jijini hapa wakati alipokuwa
amefanya ziara ya kuwatembelea wakazi hao ili kuwasikiliza na kutafuta njia ya kutatua mgogoro huo,ambapo amesema ameupokea
kwa mkono mmoja kilio cha wananchi hao kwa Waziri sumaye .
Amesema anasikitishwa
kuona mgogoro huo mpaka sasa haujapatiwa ufumbuzi huku akitoa mshangao
wake kwa kitendo cha Waziri Sumaye kutoliendeleza shamba hilo la heka 31 toka
mwaka 1991 alipolinunua mpaka sasa jambo analodai linakwenda kinyume na sheria
ya ardhi ambayo inataka mashamba yaendelezwe.
Amesema kwa sasa baada
ya kusikiliza kilio hicho ameshawasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul
Mkonda ili awasilinane na waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi,William
Lukuvi ili aweze kuja kwa wananchi hao na kutafuta ufumbuzi wa Mgogoro huo.
Amedai kuwa Mgogoro huo
ni mgeni kwake, tangu ateuliwe na Rais John Magufuli kushika nafasi hiyo kutokana
kuukuta mgogoro huo teyari ukiwa umesikilizwa na aliyekuwa mkuu wa Wilaya hiyo
ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuachiwa yeye
na akitoa ahadi ya kuumaliza mgogoro huo.
Kwa upande wa Diwani wa
Kata ya Mabwepande,Suzani Masawe amemtaka mkuu wa Wilaya kuhakikisha mgogoro
unamalizwa kwa wakati ili kuweza
kuwazesha wananchi hao kuishi kwa amani kuriko sasa wanavyoishi kwa hofu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni