Zinazobamba

MAELFU WAMUAGA MUHAMMAD ALI...AMEACHA SOMO KUBWA





Maelfu ya watu wamehudhuria swala ya Kiislamu ya kumuombea aliyekuwa mwanandondi bingwa duniani Muhammad Ali ambaye alifariki wiki iliyopita.
Swala hiyo imefanyika katika ukumbi wa ‘Freedom Hall’ katika mji aliokulia wa Louisville huko Marekani  siku ya Alhamisi. 

Waombolezaji walisikika wakimpa sifa Muhammad Ali kwa kuliita jina lake wakati mwili wa bondia huyo ulipoingizwa ukumbiniViongozi wakubwa katika ulimwengu wa ndondi na wanaharakati walikuwa sehemu ya waliohudhuria. 

Swala imeongozwa na Imam wa Alifornia, Sheikh Zaid Shakir, ambaye alikuwa pembezoni mwa Muhammad Ali pindi alipokuwa anakata roho na kupata fursa ya kumwombea dua ya mwisho kabla ya maziko

Itakumbukwa kuwa, Ukumbi wa Freedom Hall ndio sehemu ambayo pambano la mwisho la Muhammad Ali lilifanyika. Wakati huo huo , serikali ya Kongo Kinshasa imepanga kufanya sherehe rasmi ya kumkumbuka mwanandodi huyu ambaye alipambana dhidi GEROGES FOREMAN mwaka 1974, inchini humo kwa mwaliko wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mobutu Seseko.

Hakuna maoni