Zinazobamba

WALIMU TABORA WAFURIKA KLINIKI YA SAMIA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha akizungumza wakati akifungua Kliniki ya Samia ya kutatua changamoto  za Walimu iliyofanyika Ukumbi wa Isike Tabora.

*Ni Kliniki ya Samia ya kutatua changamoto za Walimu nchini.

Na Mwandishi Wetu Tabora

ZAIDI ya walimu 2000 wajitokeza kuhudumiwa Samia teachers clinik inayoratibiwa na CWT kwa kushirikiana na serikali kwa ajili ya kutatua changamoto za walimu nchini.

Ziara hiyo ya  kutatua changamoto za walimu kwa Mkoa ndio Mkoa 15 Tangu kuanzishwa kwa Kliniki ambayo inaratibiwa na Chama cha Walimu Tanzania  (CWT) kwa kushirikiana na Serikali katika kuwafikia Walimu kutoa changamoto za madai yao kwa ajili ya Serikali kufanyia kazi.

Akizungumza wakati akifungua Kliniki ya Walimu Mkoa Tabora  Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha   amesema kuwa Kliniki ya Samia hiyo itatoa suluhu ya changamoto za Walimu ya madai ya walimu kulipwa.

Amesema kuwa Kliniki ya Walimu kuanzishwa kwake ni matokeo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kwenda kutatua changamoto za Walimu kutokana na mchango wa walimu hao.

Amesema kuwa CWT ni Chama chenye nguvu na imara katika kusimamia masilahi ya Walimu na kutaka kuwa na umoja wao kushughulika katika kuendelea kuimarisha Chama.

Amesema kuwa vyama vingine zaidi ya CWT kwa viongozi hao kuendelea kuacha vyama hivyo na kuleta mawazo kujenga CWT kuendelea kuwa imara.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa Walimu wa Mkoa wa  wamejitoa sana katika kufundisha licha ya kuwa na madai  na kufanya Mkoa kuendelea kufanya vizuri katika elimu.

 Afisa Utumishi Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Judith Abdallah  amesema wamejipanga katika kutatua changamoto za Walimu katika Kliniki ya  Samia na kukutana na walimu na kuwasilisha madai yao .

Amesema kuwa walimu  wamejipanga kutoa huduma kwa idadi iliyofika huku akidai madai mengine ni maelekezo katika mifumo.Rais wa Chama cha Walimu wa Tanzania (CWT) Mwalimu Leah Ulaya akizungumza kuhusiana  na Kliniki ya Samia ya kutatua changamoto za Walimu,Mjini Tabora.

Rais wa rais wa Chama cha Walimu (CWT) Mwalimu Leah Ulaya amesema  Kliniki ya Samia wameanzisha katika kuwa rahisi ya kuwafikia walimu wakiwa na madawati ya kutoa huduma katika Wizara tano zinazoshughulika na walimu.

 Amesema kuwa Chama kimejipanga kushirikiana na serikali katika kufanya utatuzi wa madai ya walimu kukutana walimu kila Mkoa 

Aidha amesema katika kipindi hiki watashughulika na  walimu katika kuweka utulivu huku serikali ikifanya mchakato wa ulipaji wa madai yao.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Taifa Mkoa wa Tabora wa CWT Mwalimu Ally Nohoye amesema kuwa Kliniki ya Samia kuwa endelevu katika utatuzi wa changamoto za walimu.

Ameshukuru kwa kibali cha kuzunguka nchi nzima ya kusikiliza changamoto za walimu  na kwenda kufanyia kazi kwa timu inayosikiliza changamoto hizo.

Katibu wa CWT Mkoa wa Tabora Mwalimu  Condrus Stephen  amesema kuwa mwitikio ni mkubwa kwa Walimu Tabora waliofika katika Kliniki ya Samia.

Mwenyekiti  wa CWT Mkoa wa Tabora Mwalimu Emmanuel Manziriri  amesema Kliniki ya Samia ni mkombozi kwa walimu.Walimu wakiwa katika Kliniki ya kutatua changamoto yao iliyoratibiwa na CWT kwa kushirikiana  na Serikali.


Hakuna maoni