Zinazobamba

HESLB YAFANYA MBIO ZA HISANI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 20.


Na Mussa Augustine.

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB)imefanya kwa mara ya kwanza mbio za hisani katika uwanja wa Farasi uliyopo Ostabey Jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuazishwa kwa bodi hiyo mwaka 2004.

Mbio hizo za hisani za zimefanyika leo februari 15,2025 ikiwa lengo ni kuimarisha afya lakini pia  kuchangisha fedha kiasi cha shilingi milioni mia moja(Tsh.10,000,000/=) kwa ajili ya kununua vifaa vya maabara kwa shule mbili za sekondari ambapo shule  moja ipo Zanzibar na nyingine ipo bara,na kufanya maboresho katika kituo cha huduma kwa wateja cha HESLB.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwakilishi wa Baraza la Mapinduzi Dr.Hussen Ally Mwinyi,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais,Sera,Uratibu na Baraza la Uwakilishi Zanzibar Mh. Hamza Hassan Jumaa ameipongeza Bodi hiyo kwa kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake.

Waziri Jumaa amesema kwamba takwimu zinaonesha kuwa kuanzia Mwaka 2004/5 hadi sasa,Watanzania takribani laki nane wamegharamiwa masomo yao ya Elimu ya juu katika fani mbalimbali,ambapo ni ishara njema,na dhamira ya dhati ya Serikali katika kuwezesha Vijana wa kitanzania kufikia ndoto zao za kupata Elimu ya juu na kuandaa nguvu kazi ya Taifa lenye wataalamu wa fani mbalimbali hapa nchini.

"Kuwepo kwa mikopo ya Elimu ya juu kumewezesha watoto wengi wanaotoka kwenye kaya masikini kufikia ndoto za maisha yao,kule Zanzibar pia tunayo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu ambayo imetoa mchango mkubwa kwa Vijana wetu lakini hii Bodi ya Muungano imekua msaada mkubwa kwa Vijana wengi zaidi" amesema Waziri Jumaa

Nakuongeza kuwa "hivyo basi maadhimisho haya ya miongo miwili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu ni fursa muhimu ya kutathmini mafanikio yaliyopatikana nakupanga kwa ajili ya mafanikio makubwa zaidi katika siku za mbele zijazo.

Aidha amemtaka  Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia aendelee kutafuta fursa za kuongeza vyuo na kampasi za vyuo vikuu vingi kule Zanzibar vitakavyokidhi mahitaji ya vijana  ili kuendelea kuimarisha udugu  katika nyanja zote za kijamii ,kisiasa na kiuchumi kupitia uwezeshaji katika Elimu ya juu.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh.Omary Kipanga amesema kuwa mwaka 2021/22 wakati Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani bajeti ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu ilikua shilingi bilioni 464,ambapo ndani ya miaka minne ya uongozi wake imepanda  hadi kufikia shilingi bilioni 787.

"Kwa kipekee mheshimiwa mgeni rasmi tufikishie salamu zetu kwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na Dkt Hussein Mwinyi kwa kazi hii kubwa ya kupandisha bajeti ya Bodi ya Mikopo kwa zaidi ya asilimia 90,sisi kama Wizara tunajivunia,lakini tunashukuru viongozi wetu kwa utashi wao wa kisiasa kwa kuona eneo hili la Elimu ni eneo muhimu sana" amesema Mh. Kipanga 

Nakuongeza kuwa "tunaenda kufanya mapitio ya kanuni na Sheria ya Bodi ya Mikopo ( Comprehensive review) ili kutengeneza Bodi ambayo itakua ni himilivu( sustainable) katika kipindi cha miaka ishirini,miaka hamsini ijayo ambayo itaonesha katika dira yetu ya Maendeleo ya miaka hamsini ijayo namna gani Bodi yetu tunataka iwe.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Nchini (HESLB) Dkt.Bill Kiwia amesema kuwa Bodi hiyo ilipoanzishwa mwaka 2004 ilianza na wanafunzi elfu arobaini na nane tu(48,000)ikiwa na bajeti ya shilingi  bilioni 53.1,nakwamba kadri miaka ilivyokua ikisonga mbele ndivyo kiasi cha fedha kilivyokua kikiongezeka.

"Hadi kufikia mwaka 2024/25,shilingi bilioni 787 zimetolewa na Bodi kwa ajili ya wanafunzi laki mbili na elfu arobaini na tano ,mia saba tisini na tisa,(245,799),ambapo jumla ya mikopo iliyotolewa na Bodi  tangu kuanzishwa kwake ni kiasi cha shilingi trioni 8.2 ambayo imeweza kusomesha wanafunzi laki nane na elfu thelathini(8,30000)nchi nzima" amesema Dkt. Kiwia.

Maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu(HESLB)yanafikia kilele chake Februari 17 ,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Juliuasi Nyerere(JNICC )jijini Dar es salaam,ambapo mgeni rasmi katika kilele hicho anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.





Hakuna maoni