Zinazobamba

ASKOFU GWAJIMA MATATANI,POLISI WALALA NYUMBANI KWAKE,BALAA LILOMKUMBA ZITTO KABWE LAHAMIA KWAKE,SOMA HAPO KUJUA




NA KAROLI VINSENT
WAKATI Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam likitangaza kula sahani moja na Kiongozi mkuu  wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe kwa kile wanachokisema kiongozi huyo anafanya siasa za uchochezi huku wakisema mda wowote watamfikisha Mahakamani kujibu mashtaka.

Sasa Zahma hiyo limemuanguki, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima baada ya Jeshi la Polisi kuzunguka Nyumba yake iliyoko jijini hapa.

Taarifa za kuaminika kutoka kwenye Nyumba ya Kiongozi huyo wa kiroho zinasema Polisi 6 wakiwa kwenye Gari aina ya Landcruser wamefika majira ya mchana huku sababu ya kufika hapo ikiwa bado haijajulikana.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu aliyoka ndani ya Jeshi hilo ambaye hakutaka jina lake kutajwa mtandaoni kwa kile anachosema yeye si msemaji wa Jeshi hilo,amesema Sababu ya kuzunguka kwenye Nyumba hiyo inatokana na kiongozi huyo kutoa lugha anazosema ni za kichochezi.

“Ninachokwambia Ndugu huyu Askofu anamakosa mengi ila kubwa ni uwenda lugha za kichochezi, kwa maelezo jaribu kuongea na wakubwa wetu kwanza”kimesema Chanzo chetu hicho.

Fullhabari.blog ilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro ila juhudi hizo hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutopatikana.

Kufuatiliwa huku kwa wakosoaji wa Serikali kuna kuja ikiwa ni teyari Jeshi la Polisi nchini likiwa limepiga marufuku mikutano yote ya siasa pamoja na Maandamano kwa madai kuwa hali ya usalama nchini sio shwali.

Baada ya Katazo hilo,Teyari Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia Viongozi wake wakuu,wamekimbilia mahakamani wakiomba Tafsiri ya sheria juu ya katazo hilo la jeshi la Polisi,

Huku  naye alikuwa Mgombea wa Urais wa Chama hicho,Edward Lowassa amemwandikia waraka mzito wa kuhuji hatua ya Polisi kukataza Mikutano hiyo kwa kile anachokisema ni haki ya msingi wa vyama vya siasa kufanya mikutano ya kujijenga kisiasa  


Hakuna maoni