ALLY NJENJE AONYESHA NJIA YA WASANII KUPITA...AFUNGUA GROUP ZA WHATSUP NA FACEBOOK
KAMPUNI
ya Hope Light Film inayojishughulisha na uandaaji wa filamu,Documenti na
shughuli mbalimbali ambazo zinawiana na uchukuaji wa picha za mnato na video
imeunda group ambalo litaweka ukaribu baina ya wadau na mashabiki wa
filamu za Bongo Movie katika kujadiliana mambo mbalimbali katika
uendelezaji wa kazi za sanaa nchini.
Akitoa
taarifa hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook,Mkurugenzi wa kampuni
hiyo,Ally Njenje,alisema kuwa ameunda kundi la ALLY NJENJE FANS kupitia Whatsap
na Facebook ili kuwaleta pamoja wadau na mashabiki wa kazi za filamu za bongo
movie za hapa nchini pamoja na kuunganisha katika mzunguko wa biashara kwa wao
kama hope Light Film kutangaza kazi zao na kwa watu wengine pia kutangaza
biashara zao ambapo linakuwa kundi la kubadilishana mawazo ya kujiinua kiuchumi
lakini pia kusapotiana katika suala zima la biashara.
“Ndugu
zangu wadau wa Kampuni ya Hope Light Film napenda kuwajuza kuwa nimeunda group
la ALLY NJENJE FANS ambalo linaweka karibu mashabiki wa kazi zetu na kwa sababu
wewe ni shabiki wangu nami pia ni shabiki wako ambapo katika kundi hili ni
vyema kila mtu ajitambulishe kwa kazi anayofanya ili tupeane fursa wenyewe kwa
wenyewe kwa mfano nikijua wewe unafanya biashara aina fulani basi humu kaa
ukijua kuna wateja wako mmoja wapo ni mimi Ally Njenje lakini isiwe biashara
hatarishi”Alisema Njenje
Aidha
amesema kuwa watu wote watakaojiunga na kundi hilo watapata fursa ya kuwa wa
kwanza kuangalia kazi za Hope Light Film na kwa wale wote watakaokuwa tayari
kuisambaza kwenye libraly zao au zilizokuwa karibu yao au kwa wateja wowote
wale na kwa mwanakundi yeyote atakayekuwa tayari kuchukua copy kadhaa ambazo
ataenda kuziuza kwa kila copy atakayouza kutakuwa na pesa yake ni mwanakikundi
na uwezo wake wa uchakarikaji katika uuzaji wa kazi hizo.
“Ndio
maana nasema kuwa ukiwa ndani ya kundi hili utakuwa wa kwanza kuona kazi zangu
na kazi za Hope Light Film ili uangalie uzuri wake na kuangalia wapi utapeleka
kuuza kazi hizo suala hili ni la hiyari sio shuruti kwa mwenye kuiona fursa hii
ya biashara ambayo itakusaidia wewe na mimi kupata faida katika kundi hili
anakaribishwa sana”Alisema Njenje
Aliongeza
kwa kutoa nafasi kwa mtu yeyote mwenye kuona ana kipaji na ana nia ya kushiriki
katika kampuni yake kama muigizaji na akaongeza kusema kuna nafasi nyingi sana
ambazo zinahitaji watu kama uandishi wa stori za filamu,upigaji wa picha za
mnato na jongefu,kuongoza filamu,kuwafanyia make up waigizaji pamoja na kuwa
mshauri katika uboreshaji wa utengezaji wa filamu za Hope Light Film ili kutoa
kazi bora.
“Kama
unahisi ndozto zako ni kuigiza na hayo niliyoainisha hapo juu ukiwa kama kijana
au mtu wa rika lolote nakukaribisha kwenye group hili ili tufahamiane na
kusaidiana katika kujikwamua kiuchumi na kimaisha pia nataraji siku za karibuni
kuanzisha academy ya kulea watoto na watu wakubwa katika kuwajenga kisanaa kwa
kuwa naamini mimi ni msaada mkubwa kwao nitajitolea kutoa elimu ya uigizaji na
kuwapa nafasi wewe,kijana wako au ndugu yako aliyeunganishwa au kupata taarifa
hii kupitia mtu aliyejiunga katika group langu la Ally Njenje Fans kwa sababu
umenipa thamani kubwa name napaswa kukurudishia thamani hiyo”Alisema Njenje
Alimaliza
kwa kutoa wito kwa watu wote wenye kuona wanaweza kuchangamkia fursa hiyo
wajitokeze mapema kumtafuta kupitia mtandao wa facebook kwa jina la Ally Njenje
au kwa Whatsap namba yake 0713103521 na kutoa angalizo kuwa katika kundi hilo
heshima na maadili ya mtanzania yazingatiwe kwa kuwa ni katika kundi hilo
kutakuwa na watu wa rika mbalimbali na kushauri watu kuacha tabia ya kufuatana
inbox kuelezana mambo ya kijinga wengi wao katika kundi hilo wana ndoa
zao mtu anapokuchekea haimaanishi anakutaka au anastahili kusumbuliwa mtu
anapokuheshimu na yeye mheshimu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni