GAZETI LA DIRAMTANZANIA KUFUATA NYAYO ZA MAWIO,NI LILE GAZETI LINALOPAMBANA NA MAFISADI,DK MWAKYEMBE AAPA KUPAMBANA NALO,SOMA HAPO KUJUA
GAZETI la DiraMtanzania linaweza likawa Gazeti la
pili kufungia na Utawala wa awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli na
kufuata nyayo za Gazeti la Mawio ambalo nalo lilifungiwa na utawala huu.(Mtandao
huu umedokezwa).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Gazeti la DiraMtanzania ambalo ni Gazeti linalotoka
kwa wiki ambapo kwa sasa litajwa uwenda likakumbana na hali hiyo kwa kile
kinachoitwa kuandika habari zinazowachukiza “watalawa”.
Taarifa kwa za kuaminika kutoka ndani ya ofisi wa
Msajili wa Magazeti nchini ambazo Fullhabari.blog imezipata zinasema gazeti
hilo limekuwa na mwenendo mbaya ambao umeanza kuitiliwa shaka na ofisi hiyo na
kujiandaa kuchukua maamuzi magumu.
“Nakueleza kabisa baada ya Mawio hili
linafuata,kwani hata viongozi wameanza kulichukia gazeti hili kwa kuandika
habari ambazo wao wanaziona hazifai nakuhakikishia hili gazeti alifiki mbali
lazime likumbane na kibano”kimesema Chanzo chetu hicho.
Kuibuka kwa Taarifa kwa Gazeti hilo ambalo
limejipatia umaarufu hivi sasa kwa kuibua masuala ya ufisadi na kupelekea
viongozi mbali mbali wa serikali kufukuzwa kazi kutokana na habari
wanazoziandika,kuna kuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya Waziri wa Katiba na
Sheria,Dkt Harrison Mwakyembe kutishia kulipekeleka gazeti hilo mahakamani.
Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela mkoani ambaye
aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Dodoma kuwa ameshtuka na taarifa
zilizondikwa na gazeti hilo kuwa ametumia wazifa wake kujichotea zaidi ya bilioni
mbilikutoka kwa kampuni moja ya kigeni.
“Hii si mara yangu ya kwanza kutuhuma na baadhi ya habari
kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kisiasa, napenda nikiri mbele yenu kuwa sijawahi,
kushuhudia upotoshaji mkubwa na wa makusudi na uzushi uliopitiliza na chuki
binafsi iliyo bayana kama ambavyo gazeti hili limefanya,” alisema Dk. Mwakyembe na kuongeza;
“Nina taarifa kuwa, wameuza sana magazeti; naambiwa print order
(idadi ya nakala) yao imeongezeka na kwamba taarifa yao imesambaa kwenye
mitandao ya jamii, hivyo dunia nzima inajua mimi nina tuhuma za wizi, za
utapeli.”
Mbali
na Mwakyembe kusema hayo,pia teyari MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewapandisha kizimbani,
mhariri na mwandishi wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Musa Mkama na Prince
Newton kwa kosa moja la kuandika habari za uongo zilizoleta mtafaruku kwa
jamii.
Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Respicius Mwijage,
Wakili wa serikali, Timon Vitalis na Hellen Mushi, alidai mahakamani hapo kuwa,
mnamo Juni 20 katika eneo la Biafra Kinondoni, Jijini Dar es Salaam washtakiwa
hao waliandika na kuchapisha habari za uongo katika gazeti la ‘Dira ya
Mtanzania’ toleo la 424 la tarehe 20 hadi 26 ambazo zilisababisha hofu na
mshtuko kwa jamii kwa kutoa taarifa za uongo kuwa ’Kifaru cha kivita cha Jeshi la Wananchi(JWTZ), chaibwa.'
Alidai kuwa kitendo hicho ni kosa kisheria na ni kinyume na
sheria ya magazeti.
WADAU WA HABARI WANENA.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau mbali mbali
wa habari wamesema endapo Gazeti hilo likifungiwa litakuwa limeiweka picha
mbaya utawala wa serikali ya Magufuli.
‘Kama magazeti kama haya yanafichua wezi na matapeli
ya Nchi,harafu leo magazeti kama haya unayafungia,hata sifa ya kukaa jukwaani
na kusema unapambana na mafisadi teyari unakuwa umejiondolea sifa hiyo”amesema Erasto
Kaini Mwanafunzi wa Shabada ya Pili katika masuala ya Mawasiliano kwa Umma
kutoka chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Hakuna maoni
Chapisha Maoni