MAPAMBANO YAMEANZA RASMI NI KATI YA UKAWA NA CCM,SASA NI JINO KWA JINO,SOMA HAPO KUJUA
Viongozi wa Bavicha wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani |
MAMBO
yanazidi kwenda mrama kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anaandika Dani Tibason.
Msimamo uliotolewa na Baraza la
Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) unaakisi mwanzo mpya wa
msuguano wa kisiasa nchini.
Tayari
Bavicha wametangaza msimamo wa kutoshirikiana na vijana wa CCM katika tukio la
aina yoyote.
Mbali
na kutangaza msimamo huo pia wametangaza kuzuia mikutano yote ambayo
itaandaliwa na CCM kama inavyozuiwa ya Chadema.
Msimamo
huo umetolewa leo na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Bavicha wakati akizungumza na
waandishi wa habari Dodoma.
Mwita
amesema, kutokana na kitendo cha Serikali ya CCM kushirikiana na Jeshi la
Polisi kuzuia mikutano ya Chadema kinaonesha wazi kuwa, serikali ina mpango wa
kuhakikisha inaua upinzani jambo ambalo haliwezi kukubalika.
Amesema,
kutokana na hali hiyo kwa sasa Bavicha wametangaza kutoshirikiana na vijana wa
CCM katika mazingira yoyote ikiwa ni pamoja na katika masomo, nyumba
walizopanga, misiba na katika majamga mengine mbalimbali.
“Kutokana
na kuwepo kwa vitendo vya kikatili vinavyofanywa na Serikali ya CCM vya kuzuia
mikutano ya upinzani, sasa tunatangaza sisi vijana wa Bavicha hatutashirikiana
na wanachama wa CCM kwa njia yoyote ya kijamii wala kimaendeleo.
“Natangaza
kwa vijana wote wa Chadema hatutashiriki katika mazizi, hatutashiriki kusoma
nao wale waliopo katika vyuo, hatutashiriki sherehe mbalimbali zinazowahusu wao
wala hatutashiriki katika jambo lolote la kimaendeleo, na hii ni msimamo wetu.
“Pia
tunawapongeza wabunge wetu kwa kususia shughuli zote za ambazo zinafanywa na
CCM kwani kwa kufanya hivyo inaonesha kuwa sasa tumechoka na uongozi wa
kiimla,” amesema Mwita.
Hata
hivyo amedai, Rais John Magufuli ni muoga kuliko marais wote kwa kuwa ni rais
ambaye hapendi kukosolewa na kuambiwa ukweli pale ambao amekuwa akikosea jambo
ambalo anatakiwa kujitafakari na kujikosoa.
“Sasa
vijana vijana tumejipanga kuhakikisha Jeshi la Polisi linazuia mikutano au
mikusanyiko ambayo inafanywa na CCM na ikumbukwe kuwa, 23 Julai mwaka huu CCM
watakuwa na vikao vya kumkabidhi rais Magufuli kuwa mwenyekiti wa CCM.
“Sasa
tunataka Jeshi la Polisi kuzuia mkusanyiko huo na kama haitawezekana vijana wa
Chadema na Ukawa watazui mikutano hiyo.
“Haiwezekani
mikutano ya Chadema ikawa ndiyo inayozuiliwa wakati mikutano na mikusanyiko ya
CCM inaendelea kufanyika, jambo hili kamwe haiwezi kukubalika na tunasema sasa
imefika mwisho wa uvumilivu,” amesema Mwita.
Edward
Simbeye, Katibu Mwenezi Bavicha amesema, yeye ndiye mratibu wa mahafali za
wanafunzi wa Chadema vyuo vikuu (Chaso) nchini hivyo polisi walipaswa kumkamate
yeye na si kuzuia mahafali hayo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni