UTEUZI WA MAGUFULI WAVUJA,SOMA HAPO KUJUA
ASHA Rose Migiro, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa (UN), muda wowote kuanzia sasa, atatangazwa kuwa Balozi wa
Tanzania nchini Uingereza,anaandika Faki Sosi.
Taarifa za ndani kutoka katika
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa zinaeleza kuwa, jina la Dk. Migiro ambaye aliwahi kutumikia
nafasi mbalimba ndani na nje tayari limefikishwa Uingereza kwa zaidi ya mwezi
mmoja uliopita.
Hatua
hiyo imefikiwa baada ya Februari mwaka huu Rais John Magufuli kutangaza kwamba,
Dk. Migoro atateuliwa kuwa balozi bila kutaja nchi atakayokwenda kuiwakilisha
Tanzania.
Uteuzi
wa Dk. Migoro uliibua mjadala kutokana na kushika kwake nafasi mbalimbali za
kidiplomasia ambapo mjadala huo ulijielekeza kuwa ‘ameshuka ama amepanda?’
Miongoni
mwa nafasi za juu za kidiplomasia alizowahi kushika Dk. Migiro ni pamona na
kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).
Aliteuliwa
tarehe 5 Januari 2007. Dk. Migiro aliteuliwa na Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa (UN) kushika nafasi hiyo akiwa mwanamke wa pili kushika
wadhifa huo baada ya Louise Fréchette, mwanadiplomasia wa Canada aliyeongoza
kuanzia Aprili 1997 hadi Aprili 2006.
Dk.
Migiro alichukua nafasi hiyo iliyoachwa na George Mark Malloch Brown wa
Uingereza. Dk. Migiro alishikilia wadhifa huo kwa miaka mitano. Julai 2012
nafasi yake ilichukuliwa na mwanadiplomasia wa Sweden, Jan Elliason.
Mapito ya Dk. Migiro
Dk.
Migiro alizaliwa tarehe 9 Julai 1956 katika Wilaya ya Songea,
Ruvuma. Alisoma Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Dar es Salaam mwaka 1963 hadi
mwaka 1966.
Dk.
Migiro alihamia Shule ya Msingi Korogwe, Tanga ambapo aliendela na elimu ya
msingi mwaka 1967–1969.
Baadaye
akajiunga kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Weruweru,
Kilimanjaro mwaka 1970 hadi 1973 na Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya
Sekondari Korogwe mwaka 1974 -1975.
Dk.
Migiro alikuwa mmoja wa wasichana waliofaulu vizuri Korogwe Sekondari na
alipojiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1977, alichukua masomo ya
sheria na kuhitimu Shahada yake (LLB) mwaka 1980.
Baadaye
aliajiriwa UDSM kufundisha masomo ya sheria kama Mhadhiri Msaidizi. Alifanya
kazi hiyo kwa miaka miwili kabla ya kuendelea tena na masomo ya juu ya sheria
mwaka 1982–1984 hapohapo UDSM na kutunukiwa shahada ya uzamili (LLM).
Kati
ya mwaka 1985–1988, alifundisha UDSM. Mwaka 1988 alikwenda Chuo Kikuu cha
Konstanz, Ujerumani ambako alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD)
katika masuala ya Sheria mwaka 1992.
Dk.
Migiro alirejea Tanzania akiwa Mhadhiri Mwandamizi na aliendelea kufundisha
katika Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi mwaka 2000
alipoingia kwenye siasa.
Akiwa
UDSM kati ya mwaka 1992 – 1994 Dk. Migiro alikuwa Mkuu wa Idara ya Sheria za
Katiba na Utawala.
Kati
ya mwaka 1994 – 1997 aliongoza Idara ya Sheria za Makosa ya Jinai (Idara zote
zipo katika Kitivo cha Sheria UDSM).
Dk
Migiro ni mzungumzaji mzuri katika lugha ya Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani.
Ni mke wa Profesa Cleophas Migiro na wana watoto wawili wa kike.
Dk
Migiro alianza na siasa za kujijenga akitokea katika taaluma. Mwaka 2000, Rais
Mstaafu, Benjamin Mkapa alimteua kuwa waziri kwenye Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Wanawake na Watoto.
Alitumikia
wadhifa huo hadi mwaka 2005 bila kubadilishwa akisimamia mambo mengi ya kisera
na kimiundombinu, bila kusahau utekelezaji na upiganiaji wa haki za wanawake na
watoto.
Rais
Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, alimteua kuwa Mbunge na Waziri
wa Mambo ya Nje, Januari 2006 na kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia
wadhifa huo. Katika kipindi cha mwaka mmoja tu, alifanya kazi nyingi za
kimataifa zilizomweka katika anga nyingine kisiasa.
Januari
5, 2007, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu (UN) mpaka 2012 alipomaliza muda
wake. Januari mwaka 2013, Dk Migiro aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania (OUT) na Desemba 2013 aliteuliwa kuwa mbunge katika Bunge la
Tanzania.
Januari
2014 aliteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba, nafasi ambayo alidumu nayo
mpaka Rais Kikwete alipomaliza muda wake mwaka jana.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni