RAIS MAGUFULI APIGWA TENA,KAMBI YA UPINZANI,SOMA HAPO KUJUA
KAMBI Rasmi ya Upinzani imepinga tabia ya ‘kutumbua
majipu’ inayofanywa na serikali ya Dk John Magufuli hivyo imewataka watumishi
na watendaji wa umma waliosimamishwa au kufukuzwa kazi na mawaziri, kufungua
mashauri Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupinga kufukuzwa kwao na baadhi ya
mawaziri. anaandika
Regina Mkonde.
Hayo yamesemwa leo katika
hotuba ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa
2016/2017.
Kwa
mujibu wa hotuba hiyo, Lissu amesema kuwa baadhi ya mawaziri waliosimamisha na
au kufukuza kazi watumishi wa umma kwa jina maarufu kutumbua majipu, walifanya
maamuzi hayo kinyume cha sheria.
Ameongeza
kuwa Mawaziri hao hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kwa sababu
hawajakasimishwa mamlaka ya utekekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa kifungu
cha sheria cha 5(1) cha utekelezaji wa majukumu ya kiuwaziri.
Kutokana
na hali hiyo kambi ya upinzani imewataka watumishi wote ambao wametumbuliwa
wana haki na uwezo wa kwenda mahakamani na kuomba mahakama kutengua utumbuaji
wa majipu uliofanywa na mawaziri wasiokuwa na mamlaka hayo kinyume cha sheria.
“Kambi
rasmi ya upinzani inaamini kuwa kwenda kwa watumishi hao mahakamani
hakutawasaidia pekee kupata haki zao, bali pia kutakomesha vitendo vya
kuendesha nchi kienyeji na bila kufuata sheria vinavyoelekea kushamiri chini ya
utawala wa Rais John Pombe Magufuli,” amesema Lissu
Hakuna maoni
Chapisha Maoni