TRA YAWAANDALIA ZAWADI NONO WAANDISHI WA HABARI WALIOSHINDA TUZO YA UANDISHI WA KODI NA MAKUSANYO YA MAPATO,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo, kwa niaba ya
Kamishna Mkuu wa TRA (Kushoto) akimkabidhi tuzo pamoja na cheti mshindi
wa kwanza wa tuzo ya Uandishi wa
habari za Kodi na Makusanyo ya Mapato ya Serikali kwa mwaka 2015 Bi.
Valeria Mwalongo katika sherehe za kutunuku waandishi bora wa mwaka
zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam tarehe
29 Aprili 2016
Mshindi wa pili wa tuzo ya Uandishi wa habari za Kodi na Makusanyo ya Mapato ya Serikali mwaka 2015 Bw. Nuru Hassan (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo (kushoto) aliyemuwakilisha Kamishna Mkuu wa TRA katika sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam tarehe 29 Aprili 2016
Mshindi wa pili wa tuzo ya Uandishi wa habari za Kodi na Makusanyo ya Mapato ya Serikali mwaka 2015 Bw. Nuru Hassan (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo (kushoto) aliyemuwakilisha Kamishna Mkuu wa TRA katika sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam tarehe 29 Aprili 2016
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tuzo za
Umahiri katika Uandishi wa Habari, ambazo hutolewa na Baraza la Habari Tanzania
(MCT), waandishi wawili wameshinda tuzo ya Uandishi
wa Kodi na Makusanyo ya Mapato ya Serikali kwa mwaka 2015,
Waandishi hao wawili, Valeria Mwalongo, mwandishi wa
Redio Tumaini aliyeshika nafasi ya kwanza na Bw. Nuru Hassan kutoka Afya Redio
aliyeshika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro hicho ni washiriki na washindi
wa kwanza kupata tuzo hiyo ambayo imeingizwa kwa mara ya kwanza kwa kazi za mwaka
2015.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka
TRA Bw. Richard Kayombo alitoa tuzo hiyo kwa waandishi hao kwa niaba ya
Kamishna Mkuu wa TRA katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam ambako sherehe
za kutunuku Zawadi zilifanyika.
Kutokana na
ushindi huo Bw. Richard Kayombo amesema TRA itatoa donge nono kwa waandishi wa
habari watakaoshiriki na kushinda katika kundi la uandishi wa habari za kodi na
ukusanyaji wa mapato. Mshindi wa kwanza wa 2015 Bi. Valeria Mwalongo atajipatia
kompyuta mpakato na wapili Bw. Nuru Hassan atajipatia simu aina ya Samsung
mbali na kupata tuzo na vyeti kutoka MCT.
“Mamlaka ya
Mapato Tanzania imedhamiria kuwajengea uwezo zaidi wanahabari kwa kuwaelimisha
juu ya masuala ya kodi kwa kushirikiana na MCT ambao wao
watawajengea uwezo juu ya
uandishi bora kwaajili ya kuchochea ushindani zaidi katika kundi hili mwaka
ujao kwa kazi ambazo zitaandikwa katika mwaka huu wa 2016.” Alisema Bw. Kayombo
MCT ilianzisha kundi la tuzo za uandishi wa habari
za kodi na ukusanyaji mapato baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kuomba kundi
hili liingizwe katika tuzo hizo kwa kuzingatia kwamba waandishi na watangazaji wa
habari wanaweza kushiriki kwa kuandika masuala ambayo yataongeza ridhaa ya
kulipa kodi kwa hiari.
Sehemu ya barua ya TRA kwa MCT inasema, “TRA
inatekeleza majukumu mbalimbali na mojawapo ni kuihabarisha jamii kupitia
vyombo mbalimbali. TRA pekee haiwezi kufanikisha jukumu hili bila
kuwashirikisha wadau ndio maana inaiomba MCT kuanzisha kundi la tuzo ya
uandishi wa masuala ya kodi”
Tuzo ya kundi la
uandishi wa Kodi na ukusanyaji mapato ya serikali ilijumuisha
habari mbalimbali za masuala ya kodi, masuala ya ukusanyaji wa kodi, umuhimu na matumizi ya
kodi hasa katika kugharimia huduma za jamii, nidhamu ya ukusanyaji na utumiaji,
mianya ya upotevu wa mapato, njia za kuongeza wigo wa kodi. Nia ni kuongeza
uhiari wa ulipaji kodi kwa ili kukuza
mapato ya serikali
MCT ilizindua uwasilishaji wa kazi za wanahabari
tarehe 12 Februari 2016 kwa makundi 22 yaliyojumuisha uandishi wa habari za Uchumi na Biashara, Michezo na
Utamaduni, Mazingira, Watoto, Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, Utawala Bora,
Jinsia, Sayansi na Teknolojia, Afya ya Uzazi, Uandishi wa Uchunguzi, Elimu,
Utalii na Uhifadhi, walemavu, Mpiga picha bora wa magazeti, Mpiga picha bora,
Mchoraji kibonzo bora, Afya ya Uzazi kwa Vijana, Gesi, petrol, Utafiti wa Madini
pamoja na habari za kodi na ukusanyaji mapato.
TRA inatoa wito
kwa waandishi wote kujitokeza kwa wingi zaidi kuwania kinyang’anyiro hiki
katika mashindano ya mwaka ujao ili kuendelea kupaza sauti juu ya masuala
mbalimbali yahusuyo kodi na kujishindia zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa
kipindi hicho.
“Pamoja
Tunajenga Taifa Letu”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni