SERIKALI RAIS SHEIN YACHAFUKA,MSHAURI WAKE AKUTWA AKILA URODA NA MWANAKE,SOMA HAPO KUJUA
SERIKALI ya Dk. Ali Mohammed Shein
imezama kwenye aibu, ni baada ya mshauri wake Dadi Faki Dadi kukamatwa kwa
tuhuma za kufanya ngono na mwanaye, anaandika Pendo Omary.
Faki alikuwa Mkuu Mkoa wa Kaskazini Pemba lakini baada ya kukosa
nafasi hiyo katika ngwe ya pili ya Dk. Shein, aliteuliwa kushika nafasi hiyo ya
ushahuri kwa rais hususan masuala ya yanayohusu Pemba.
Mshauri huyo
amekamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na mtoto wake wa kambo (mtoto wa mkewe)
mwenye umri wa miaka 21.
Mwanasiasa huyo
maarufu visiwani humo alikamatwa mbele ya mkewe na baadhi ya wanafamilia juzi
katika nyumba ya wageni ya Executive, jirani na Makao Makuu ya Uhamiaji
Zanzibar, eneo la Kilimani mjini Unguja na kupelekwa katika kituo cha Polisi
Mwembemadema.
Mkadam Khamis,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi amethibitisha kushikiliwa kwa Dadi na
polisi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana wakati uchunguzi wa tukio hilo
ukiendelea.
“Tunaendelea
kufanya uchunguzi. Iwapo tutabaini ametenda kosa tutampeleka katika vyombo vya
sheria,” amesema Khamis.
Aidha, picha za
video ambazo zinaendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii zinamuonesha
Dadi akishambuliwa kwa maneno makali kutoka kwa mkewe na watu waliomkamata.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni