BARAZA LA WAZEE LA YANGA LAIKOMALIA TFF NA BMT,SOMA HAPO KUJUA
BARAZA la Wazee la Klabu ya soka ya Yanga limelitaka
shirikisho la Soka nchini (TFF) pamoja
na Baraza la michezo nchini (BMT) kutoa ufafanuzi wa haraka kuhusu kadi gani
hasa zitumike na wanachama wakati wa kupiga kura kwenye uchaguzi wa Klabu hiyo .,Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Ombo hilo limetolewa na Katibu mkuu wa Baraza
hilo,Ibrahimu Akilimali wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini
Dar es Salaam, amesema Wazee hao wameshtushwa na Tamko lilotolewa na Tff pamoja
BMT linalowataka wanachama wa Yanga wanaorusiwa kupiga kura kwenye uchaguzi huo
ni wale tu wenye kadi za zamani za Yanga
na sio vingenevyo.
Amesema Tamko hilo linawapa shida wanachama kwa
madai kuwa kwa sasa hivi wapo wanachama wenye kadi za Posta ,kutokana na
wanachama wengi wa kadi za zamani wamebadilisha kadi zao na kwenda kwenye kadi
za Posta.
Mzee Akilimali amebainisha kuwa kitendo cha
kuwabagua wale wenye kadi za zamani ndio wapewa haki ya kupiga kura na kuwaacha
wenye kadi za Posta ni kitendo ambacho wanadi kuwa kitaleta mgogoro mkubwa katika Klabu hiyo ambayo ni Mabingwa wa Kombe
la Ligi.
Amesema kitendo cha kuwaruhusu wanachama wenye kadi
mbili kupiga kura sio kitu kigeni kwenye Klabu hiyo huku akitolea mfano uchaguzi wa mwaka 2006
kwa Yanga asili na Yanga Kampuni walivyotoa uongoa harali.
Hata Hivyo,Akilimali ameliomba BMT pamoja TFF
kuiruhusu sekretarieti ya Yanga kuitisha mkutano mkuu wa Dharula wa wanachama ambao utakuwa na ajenda ya
Uchaguzi mkuu ili wanachama wapewe taarifa kuhusu uchaguzi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni