IGP MWEMA AMEKWISHA,KASHFA YA UFISADI WA LUGUMI KUMMALIZA,WABUNGE WAJIAPIZA,SOMA HAPO KUJUA
Ni Mungu tu ndiye atayeweza mwokoa alikuwa Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini,IGP Said Mwema kwenye Kashfa ya fisadi katika mkataba kati ya Kampuni ya Lugumi
Enterprises Ltd na Jeshi la Polisi ndivyo naweza kusema kutokana kutajwa kuhusika kwake.(Mtandao
huu umedokweza).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kwa mujibu wa chanzo
cha kuaminika kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)
ambapo Kamati hiyo ilikuwa na kazi moja tu,ya kuchunguza Kampuni hiyo ambapo
kwa sasa kazi ya uchuguzi huo umekamilika kwenye mikoa tofauti nchini na kinachosubiliwa ni kukabidhi ripoti hiyo kwa Spika ili isomwe kwa wabunge,
Ambao chanzo
chetu hicho kimeiambia Fullhabari.blogs kuwa Kamati hiyo
imebaini madudu ambayo yanamweka pabaya IGP Mwema.
“Ninachokwambia
Ndugu,yaani tumebaini madudu mengi,ambayo kama wabunge wa CCM wakiacha mtindo
wao wakukitetea chama basi,huyu IGP Mwema achomoki,kwasababu ni mtu ambaye
anatakiwa kuchunguzwa mara moja na taasisi za kuzuia rushwa kama TAKUKURU,”Kimesema
Chanzo chetu hicho.
Ametaja kinachomweka
Pabaya IGP Mwema ambaye wakati mkataba wa Lugumi unaingiwa alikuwa IGP ni kitendo chake cha kuhusika au kuwanyamazia
viongozi wandamizi wa Jeshi la Polisi mpaka kupa tenda Kamapuni ya Lugumi
kwenye Mkataba wa Bilioni 39 huku ikiwa haina sifa wala mtaji wa kuweza
kutekeleza kazi hiyo.
“Yaani hii kampuni
inautata sana,tumeibani kuwa haina sifa hata moja,harafu katika uingiaji wake
mkataba na jeshi la Polisi inatokana shinikizo la huyu bwana (Mwema),kwa vyovyote
vile kamati hii ikisomwa kwa wabunge nakuhakikishia utasikia makubwa na tumeapa
kupambana mpaka haki itendeke,tumechoka kusikia tunatoa mapendekezo kama kwenye
Escrow harafu tunapuuzwa,kwa sasa hatutakubali “kimezidi sema Chanzo chetu
hicho.
Kuibuka kwa taarifa
hii kuna kuja ikiwa wiki mbili baada ya Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema wakati akiwasilisha maoni ya Kambi ya
Upinzani Bungeni kwenye Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi ambapo Mbunge huyo alisema Kampuni ya Lugumi imepewa tenda
huku ikiwa haina sifa pamoja na kujaa upendelea mtupu wakati utoaji tenda.
UTATA WA KAMPUNI YA LUGUMI.
Kampuni ya Lugumi inadaiwa kupewa tenda na jeshi hilo kwa ajili ya
kufunga mashine za kuchukua alama za vidole – ‘Biometric Access’ katika vituo
108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.
Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 pekee na tayari kampuni
hiyo imelipwa Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha zote za
mkataba.
Katika sakata hilo, inadaiwa Kampuni ya Lugumi ilipewa zabuni hiyo
ikiwa haina uzoefu wa kazi hiyo.
“Wamepewa mkataba sawa, lakini mbona taarifa zinaonyesha kuwa kampuni
hii haijasajiliwa kama Biometric Access Company na haijawahi kufanya kazi
zozote zinazohusu Biometric Access Control?” alihoji mmoja wa wataalamu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni