ASKOFU MALASUSA ANAZIDI ZAMA,KASHFA LUKUKI ZAMTAFUNA,SOMA HAPO KUJUA
DK. Alex Malasusa, Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), ameanza
mchakato wa kubadilisha katiba ya kanisa lake ili kuzuia kung’olewa madarakani. Anaandika Mwandishi Wetu.
Askofu Dk. Malasusa amelenga
kubadilisha katiba ya kanisa hilo ili kuzuia mkuu mpya wa KKKT, Frederick Shoo,
kuingilia kati mgogoro unaofukuta ndani ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Taarifa
kutoka ndani ya kanisa hilo zinasema, Kamati Maalum ya mabadiliko ya katiba,
tayari imeelekezwa kuondoa ndani ya katiba ya DMP, kifungu kinachoipa nguvu
KKKT na mkuu wake kuingilia mgogoro wowote wa kanisa hilo na kumchunguza askofu
wa dayosisi hiyo.
Mabadiliko
ndani ya DMP yanafanyika takribani miezi mitano baada ya Askofu Dk. Malasusa
kuondolewa katika wadhifa wa mkuu wa KKKT.
Aidha,
mabadiliko ya katiba ya kanisa la Askofu Dk. Malasusa yanakuja miezi mitatu
tangu kiongozi huyo kutuhumiwa kujihusisha kimapenzi na mchungaji wa kanisa
lake na ambaye ni mke wa mtu.
Anayetajwa
kuwa na uhusiano wa kingono na Dk. Malasusa, ni Leita Ngowi, mchungaji na
mkurugenzi wa idara ya wanawake usharika wa Azania Front, jijini Dar es Salaam.
Leita
ni mke wa Venance Mwakilima, mkazi wa eneo Vikawe, Bagamoyo, ambaye ni
mfanyakazi wa Shule ya Msingi Dunda, wilayani Bagamoyo.
Dk.
Malasusa anadaiwa kuwa na uhusiano na aliyepandishwa cheo siku za karibuni na
askofu huyo.
“…huyu
bwana (Askofu Malasusa) anahofia kuwa uchunguzi ukifanyika kama ambavyo baadhi
ya wachungaji wameomba kwa mkuu wa kanisa, uchafu wake utajulikana,” ameeleza
kiongozi mmoja ndani ya DMP.
Anasema,
“hakuna haja ya kuwa na mabadiliko ya aina hiyo. Wala hakuna haraka ya
marekebisho ya katiba, wakati marekebisho ya mwisho yalifanyika miaka miwili
iliyopita.”
Akiongea
kwa uchungu mtoa taarifa huyo anasema, “…anataka kufanyia mabadiliko katiba
yetu ili kuzuia asiweze kuchunguzwa. Sisi wengine tunamshangaa sana, kwa nini
dhambi ya watu wawili tunabebeshwa kanisa zima?”
Taarifa
zinasema, ni kawaida kwa katiba ya DMP kubadilishwa kwa manufaa ya mtu binafsi.
Mara
ya mwisho mabadiliko kwenye katiba ya DMP yalifanyika ili kumuondoa mchungaji
mmoja ambaye alipendekezwa kuwa msaidizi wa askofu.
Anasema,
“katika mabadiliko yake, Askofu wa DMP amepewa mamlaka makubwa ya kuteua
msaidizi wake; kwa sasa msaidizi wa Askofu, ni kama anapendekezwa na Askofu
kisha kuthibitishwa na mkutano mkuu.”
Kabla
ya mabadiliko hayo, msaidizi wa Askofu alikuwa anapendekezwa na kamati mahususi
ya uteuzi inayotokana na Halmashauri Kuu ya Dayosisi.
Akiongea
katika mkutano wa watumishi ulioitiswa kwa dharura ili kushawishi “watumishi
kuwa na kauli moja” juu kile kinachoitwa, “yanayoendelea kwenye magazeti kuhusu
Askofu Malasusa,” msaidizi wa Askofu huyo alidai, yote yanayoandikwa kuhusu
bosi wake, “hayana ukweli.”
Alisema,
“haya mambo yanayoandikwa kwenye magazeti kuhusu mkuu wa kanisa ni uzushi na
uongo mtupu.”
Hata
hivyo, msaidizi wa Askofu alizuia wauamini kuhoji kwa nini magazeti yameamua
kumuandama Askofu Malasusa wakati huu na siyo wakati alipokuwa kiongozi mkuu wa
KKKT.
Aliishia
kuwataka wajumbe kufanya maombi kwa kanisa na kiongozi wao.
Wakati
msaidizi wa Askofu Malasusa akieleza wajumbe anachoita, “uongo wa magazeti,”
Mchungaji Leita alikuwa ameketi mbele na viongozi wengine wa dayosisi hiyo.
Alikuwa
kimya, mwenye majonzi na aliyeonekana kuwa na kitu kinamsumbua moyoni mwake.
Mwandishi
wa habari hii aliyefanikiwa kujipenyeza ndani ya mkutano huo alimnukuu mmoja wa
wutumishi akilalamikia namna ya viongozi wa dayosisi hiyo wanavyolishughulikia
suala hilo.
“Wamefanikiwa
kuwatiisha baadhi ya viongozi wa DMP, lakini hawatafanikiwa kutuziba mdomo
wengine. Hatuwezi kukubali kuwa makasuku kwamba eti kashfa ya askofu ni ya
kitaasisi na siyo binafsi,” ameeleza Mchungaji mmoja ambaye hakupenda kutajwa
jina.
Akiongea
kwa hisia kali, mchungaji huyo alisema, “… uzinzi unawezaje kuwa wa taasisi?
Hawa watu wanazungumza kama wasiofahamu Biblia?
“Ndani
ya Bibilia, kumeandikwa kuwa Mfalme Daudi alimuua Uria, ambaye alikuwa Jemedari
wake wa vita. Mungu hakuifanya dhambi ile kuwa ya Israel. Alimwadhibu Daudi na
sio taifa zima. Hatuwezi kuifanya dhambi ya Askofu Malasusa kuwa dhambi ya
kanisa zima. Haiwezekani.”
Akizungumza
katika mkutano huo, mchungaji Ernest Kadiva, naibu katibu mkuu utawala,
alitangaza kuanza kwa mchakato wa mabadiliko ya katiba ya DMP, kwa kusema
“hautafanyika kupitia vikao mahususi kama ilivyozoeleka.”
Mchungaji
Kadiva ambaye likuwa pia mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba alisema, mabadiliko
ya ya Katiba ya DMP yanayofanyika sasa, “yanataka kila mwenye maoni kuwasilisha
mapendekezo yake kwa maandishi” kwake.
Mabadiliko
haya ya katiba ya DMP yakifanyika, utakuwa “ushindi mkubwa” kwa Askofu
Malasusa. Atakuwa amefanikiwa kufanya mambo mawili:
Kumzuia
kisheria Askosu Shoo kushungulikia mgogoro mkubwa unaofukuta katika kanisa lake
na kuzuia kuumbuliwa katika kashfa ya ngono inayomkabili.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni