Mstahiki Meya Halimashauri Wilaya ya Ilala Charles Kuyeko.
Kasumba ya wahudumu wa hospitali na zahanati za serikali kuwapuuza wagonjwa na kupelekea wagonjwa hao kuwa na hali mbaya na wengine kufikwa na umauti kwa uzembe wao jambo ambalo limekuwa kero kwa wananchi mbalimbali nchini.
Tukio la aina hiyo limetokea usiku wa Ijumaa katika Hospitali ya Amana baada ya ndugu wa marehemu Nassoro Hamis (Dereva Bodaboda) kumpeleka ndugu yao katika hospitali hiyo na kupuuzwa na baadhi ya wahudumu wa hospitali hiyo kwa kile kinachodaiwa hawakuweza kulipa mchango wa kadi ambao ni shilingi 20000 hali ya kuwa mgonjwa alikuwa katika hali mbaya baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa kwa risasi na majambazi.
Uzembe huo wa wahudumu umepelekea kifo cha Nassoro Hamisi jambo ambalo limemsikitisha Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko na kuamua kumuagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri wa Wilaya hiyo Victorina Ludovick kuwachukulia hatua za kinidhamu wote wanaohusika na uzembe huo uliopelekea kifo cha dereva bodaboda na kuahidi kulifu
Aidha Mstahiki Meya Charles Kuyeko ameongeza kuwa endapo matukio ya namna hiyo yataendelea kujitokeza katika hospitali zilizo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilala, watachukua hatua za kuwafungia leseni za kutoa huduma Madaktari na Wahudumu wa Afya wenye hulka za namna hiyo.
atilia suala hilo kikamilifu.
MEYA WA UKAWA ILALA AINGILIA KATI UNYAMA HUU,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
16:31:00
Rating: 5
Hakuna maoni
Chapisha Maoni