WANAHABARI WAUCHOKA UTAWALA WA MAGUFULI MAPEMA,JUKWAA LA WAHARIRI NAO WAUJIA JUU,SOMA HAPO KUJUA
SERIKALI ya Rais John Magufuli inalalamikiwa
kutokana na serikali yake kujenga tabia ya ukandamizaji kwa wanahabari, anaandika Moses Mseti.
Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF) limeeleza kusikitika kutokana na kujengekwa kwa tabia hiyo na kwamba,
kitendo cha kunyang’anya uhuru na haki ya wananchi kupata habari hakikubaliki
Makamu
Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amesema, kutokana na ukandamizaji unaofanywa
na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli hauvumiliki.
Moja
ya mambo na sheria zinazoonekana kuvikwaza vyombo vya habari nchini ni
waandishi wa habari kuzuiwa kuchukua habari moja kwa moja ‘live’ wakati wa
vikao vya bunge la bajeti na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 pia
kutungwa kwa sheria zinazokandamiza vyombo vya habari na waandishi wake.
Akizungumza
leo wakati wa kilele cha Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) amesema, kitendo cha
serikali kuwazuia waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonesha ‘live’
bunge hilo ni sawa na uvunjwanji wa Sheria na Haki ya Kupata Habari huku akidai
kitendo hicho hawakubaliani nacho.
“Mwaka
1992 sheria za habari zilikuwa 17 lakini sasa hivi zimetengenezwa tengenezwa tu
hadi kufikia 26 hiyo yote ni ya Serikali kutaka kuvibana vyombo vya habari
visifanye kazi zao kwa uhuru, kitendo ambacho ni kibaya sana kwa ukuaji wa
tasnia hii,” amesema Balile.
Pia
Balile ametolea mfano sheria ya takwimu (The statistics act, 2013) ambayo
anasema kuwa, sheria hiyo ipo kwa lengo la kumkandamiza mwanahabari na vyombo
vya habari.
Na
kwamba, kwenye kutekeleza wajibu wao na hawatarudi nyuma katika kutetea suala
hilo mpaka pale litakapopatiwa ufumbuzi.
“Mfano
kuna hili suala la takwimu ambalo linawanyima waandishi wa habari, kwamba kama
mwandishi akiandika takwimu ambazo zitakuwa zimekosewa na mtoa taarifa, yeye ndie
anaekuwa mhanga tatizo na wakati yeye kaandika,”alisema Balile.
Katika
hatua nyingine Ubalozi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania umeeleza mambo
17 yanayolenga kulisaidia Taifa kupiga hatua ya maendeleo pamoja na vyombo vya
habari nchini kukuwa kitaaluma kwa miaka 10.
Akiwasilisha
malengo hayo 17 kwa wahariri, waandishi wa habari na wadau wa habari, Usiah
Nkoma, Ofisa Habari UN amesema, malengo hayo yanakusudia kuleta maendeleo
endelevu ya kiuchumi.
Nkoma
ameyataja mambo hayo kuwa ni kutokomeza umaskini, kukomesha njaa, afya njema na
ustawi, elimu bora, usawa wa jinsia, maji salama na safi, nishati mbadala kwa
gharama ndogo, kazi zenye staha na ukuzaji uchumi.
Pia
ametaja mambo mengine kuwa ni kukuzaviwanda na miundombinu, kupunguza tofauti
za kiubinadamu, kuwa na miji na jamii endelevu, matumizi na uzalishaji wenye
uwajibikaji, kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, kuendeleza uhai
katika maji.
Nkoma
ametaja mambo mengine kuwa ni pamoja na kulinda uhai wa ardhi, amani, haki na
taasisi madhubuti na ushirikiano katika kufanikisha malengo hayo endelevu kwa
ukuaji wa uchumi wa taifa na vyombo vya habari kwa ujumla.
“Malengo
yetu nikuona kila mmoja akiwajibika kwa nafasi yake na waandishi wa habari
kwenye taifa lolote lile wao ndio nguzo kubwa kwa ukuaji wa maendeleo yaTaifa
hilo ni lazima kuwepo na mazingira salama,” amesema Nkoma.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni