MAGDALENA SAKAYA WA CUF ALIA NA RUSHWA KWENYE KILIMO,SOMA HAPO KUJUA
Magdalena Sakaya, Waziri Kivuli katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi |
WATENDAJI katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
wameelezwa kuingia mikataba ya ovyo kwenye baadhi ya Vyama vya Ushirika ikiwa
ni pamoja na usimamizi mbovu, anaandika Regina Mkonde.
Magdalena Sakaya, Waziri Kivuli
katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi amesema hay oleo wakati akitoa hotuba
kuhusu mapitio ya utekelezaji wa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 na
makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa 2016/2017 mjini Dodoma.
Wakati
akisoma hotuba hiyo, Sakaya amesema kuwa, Vyama vya Ushirika vya kilimo nchini
viko katika hali mbaya kiuchumi kwa kuwa, Maofisa Ushirika wenye jukumu la
kufanya ukaguzi kisheria kwenye vyama vya ushirika, wameshindwa kutimiza wajibu
huo huku baadhi yao wakishirikiana na viongozi wa ushirika kuhujumu vyama
hivyo.
“Kutokana
na ubadhirifu mkubwa uliojitokeza kwenye vyama vya ushirika vya Mkoa wa Tabora
kuanzia chama kikuu WETCO, Serikali kupitia aliyekuwa waziri mwenye dhamana ya
kilimo Prof. Jumanne Maghembe iliagiza kufanyika ukaguzi maalum Mkoa wa Tabora
na taarifa ikapatikana,” amesema na kuongeza;
“Kambi
rasmi ya upinzani inauliza je, ni kwa nini hadi leo wahusika wa ubadhirifu huo
hawakuchukuliwa hatua? Serikali inaliambia nini bunge hili?
“Agizo
la waziri kuwa wahusika wafikishwe mbele ya sheria mbona halijatekelezwa hadi
sasa?”
Kwa
upande wa kunufaisha wakulima wa zao la tumbaku ameeleza kuwa, mwaka wa fedha
wa 2014/2015 wakati waziri aliyekuwa na dhamana ya kilimo alipokuwa
akiwasilisha bajeti yake.
Amesema
kuwa, serikali ilitafuta wanunuzi wa tumbaku kutoka Korea na China ili kuongeza
ushindani kwa kampuni zinayonunua tumbaku kutoka kwa wakulima jambo ambalo
halijatekelezwa hadi sasa.
“Kambi
rasmi ya upinzani inataka kujua utekelezaji wa mpango huu umefika wapi?
Wanunuzi hao wameshafika au bado wako njiani?
Sakaya
ameeleza kuwa, mashamba mengi ambayo yalikuwa yanamilikiwa na serikali
yaliyokuwa yanazalisha vizuri ambayo serikali iliamua kuingia ubia au kuyauza.
Mikataba
mingi ya ubia iliingiwa bila kuzingatia masilahi ya Taifa na badala yake
ilizingatia zaidi masilahi binafsihuku akitaja mifano ya mikataba hiyo ikiwemo
mikataba ya ubia ya Kampuni ya Kilombero Plantations Ltd (KPL) na Mgololo.
“Mkataba
ulioingiwa na serikali kupitia RUBADA na kampuni ya KPL ambapo kabla ya mkataba
huo RUBADA ilikuwa na mbia mwingine wa Kikorea akiitwa Kotako ambaye alikuwa na
majengo, mashine za uzalishaji, matrekta, magari, na mashmba ya mngeta,”
amesema na kuongeza;
“Lakini
kwa sasa baada ya Kotako kuondoka maana yake RUBADA ndiye mmliki wa hisa
asilimia 5 na KPL wanamiliki hisa 95 ambao hawakuwekeza zaidi ya kukuta kila
kitu site na kuanza kuuza na kukodisha mashine na mashamba kwa wakulima.”
Sakaya
amesema kwamba, Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kuwa sasa ni muda muafaka wa
kuiangalia na kuipitia upya mikataba yote iliyokuwa imeingiwa na serikali na
wawekezaji na kuona kama kweli ina masilahi kwa nchi au iliangalia zaidi
masilahi binafsi kutokana na kugubikwa na ufisadi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni