SUMAYE AMPOPOA MAGUFULI,BAADA YA SERIKALI YAKE KULIFANYA BUNGE KUWA "GIZANI",SOMA HAPO
Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu |
FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu ameeleza
kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na
kuchukia kukosolewa, anaandika Pendo Omary.
Sumaye bila kumtaja jina Rais
Magufuli ameleza kushangazwa na hatua ya serikali kuminya uhuru wa habari na
kwamba, kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu yanayofanywa na watendaji wake.
“Wapowatawala
ambao hawapendi kusemwa lakini wanapenda sana kusifiwa. Kiongozi mwenye tabia
ya udikteta hataki kusikia kingine zaidi ya sifa zake tu.
“Huyo
ni mtu hatari na katika nchi ya namna hiyo hakuna uhuru wa habari wala uhuru wa
kutoa maoni kwa woga wa kupotezwa kusikojulikana,” amesema Sumaye.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habri za
Siasa (TAPOREA), Sumaye amesema, serikali inakiuka Katiba ya nchi.
Amesema,
serikali yoyote inayopambana na vyombo vya habari na kuminya uhuru wa kufanya
kazi zao huwa ina tatizo kwa upande wa wanaotawala.
Akitolea
mfano wa hatua ya serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge Sumaye
amesema, kwa kufanya hivyo serikali imevunja Katiba.
“Unapoondoa
matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya Bunge, kwanza ni kuvunja katiba.
Ibara ya 18 (d) ya Katiba inasema, kila mtu ana haki ya kupewa taarifa wakati
wote.
“Kwa
kuzuia Bunge kuoneshwa ‘live’ (moja kwa moja) wewe serikali unataka kutoa
taarifa ya Bunge kwa wakati unaoutaka na kwa taarifa unayoitaka wewe,” ameeleza
Sumaye.
Kuhusu
sababu iliyotolewa kwamba, matangazo hayo yanatumia gharama ya Sh. 4 bilioni
amesema haina mashiko.
Sumaye
amesema, hata kama matangazo hayo yatarushwa na ofisi za bunge bado, gharama
zitaongezeka zaidi kwa sababu Bunge litahitaji kununua mitambo pamoja na
kuajiri wafanyakazi wake.
Sumaye
amesema, serikali yenye demokrasia ya kweli lazima ikubali wananchi wake kutoa
maoni.
“Serikali
yoyote yenye utawala bora, ingependa mambo yake inayoyafanya kwa ajili ya
wananchi wake mambo hayo yajulikane kwa wananchi hao.
“Ukiona
serikali inaficha mambo yake lazima kuna mambo wanayoyafanya ambayo hayafai na
wasingependa jamii ijue,” amesema Sumaye.
George
Maziku, Mkurugenzi Mtendaji wa TAPOREA amesema, ripoti ya hali ya uhuru wa
waandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari kimataifa, iliyotolewa na
Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka lenye Makao Makuu yake nchini
Ufaransa haipendezi.
Amesema,
ripoti hiyo inaonesha kuwa, katika miaka 10 iliyopita zaidi ya waandishi wa
habari 800 kutoka mataifa mabalimbali duniani wameuawa wakiwa wanatekeleza kazi
zao.
“Kitisho
kingine kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini ni utamaduni mpya ulioasisiwa na
kuimarishwa na watawala wa sasa na kuvishinikiza vyombo vya habri kutomkosoa
Rais John Magufuli na serikali yake.
“Matokeo
yake, vyombo vingi vya habari nchini vimelazimika kuandika habari za
kumfurahisha Rais Magufuli,” amesema Maziku.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni