MADIWANI WA MANISPAA YA KINONDONI WAITILIA SHAKA SERA YA ELIMU BURE,SOMA HAPO KUJUA
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob (katikati) akiongoza sala ya kufungua mkutano wa baraza la Madiwani wa manispaa hiyo. |
NA KAROLI VINSENT
MADIWANI wa
Manispaa ya Kinondoni wametilia shaka hatua ya serikali kutangaza elimu bure
kwa madai kuwa kiasi cha fedha kinachotengwa kwenda kwenye shule kwa ajili ya
kuhudumia sera hiyo ni kiasi kidogo.
Madiwani hao bila kujaliitikadi zao za vyama,
wameyasema hayo leo wakati wa kikao cha baraza la madiwani ya Halmashauri ya
Kinondoni,
Eprahim Kinyafu diwani wa kata ya Saranga kwa kiketi ya
Chama cha Demokrasia Chadema amesema kiasi cha fedha cha Bilioni 4 zilizotengwa
na Halmashauri hiyo kwa mwaka kwenda kusaidia elimu bure ni kiasi kidogo
hakiwezi kukidhi mahitaji ya wanafunzi.
Amesema kiasi hicho kidogo kimewafanya walimu
kushindwa kuwahaudumia wanafunzi huku akitolea mfano kiasi kidogo cha Laki tatu
kinachotegwa kwa kila shule kwa ajili ya kuwalipa walinzi akisema
Naye Diwani wa Kata ya Mwananyamala Songoro Mnyonge
CCM amesema kuwa hadhani kuwa kwa kusema ukweli kama Magufuli atamtumbua ila
akiweka itikadi yake pembeni, ufaulu wa wanafunzi utaporomoka sana kutokana na
fedha hizo kuwa ndogo kiasi cha kuto kidhi mahitaji ya shule husika.
Imeelezwa kuwa kila mwezi Hazina hutuma shilingi 548
kwa kila mwanafunzi fedha ambayo pia haifiki kwa wakati shuleni na kufanya
mahitaji ya mhimu kukosekana huku Raisi akisisitiza wazazi kutochangishwa.
Mahitaji mhimu kwenye shule ni chaki, posho za
walinzi, maji kwa ajili ya matumizi ya vyoo, umeme, siteshenari, na vitu
vingine.
Aidha imeelezwa kuwa kwa kawaida kila mwanafunzi
anatakiwa kupata shilingi 10000 kwa mwaka lakini shuleni inafika shilingi 6000
tu huku shilingi 4000 ikienda TAMISEMI kwa ajili ya kununulia vitabu.
DiwaniMichael Urio wa Kunduchi alisema kuwa majibu
toka kwa watendaji wa Halmashauri kila siku hayaridhishi na yamekinzana sana
kutokana na usiri uliogubika fedha hizo na kuwataka watendaji hao kutoa taarifa
ya fedha hizo kila mara kwenye vikao vya Baraza hilo.
“Majibu hayo mkurugenzi hayaridhishi kutokana na
tarifa zake kugubikwa na usiri mkubwa tunaomba kuanzia sasa tuwe tunapewa kila
mara ili tukienda kukagua huko mashuleni tuweze kusimamia” alisema Urio.
Aidha madiwani hao wameeleza kuwa shule nyingi
katika Manispaa ya Kinondoni zinakabiliwa na uhaba wa vyoo na nyingine zimeshafungwa
katika Kata ya Makuburi kutokana na uhaba wa matundu ya vyoo na wananshangaa
Serikali inaangalia madawati tu.
Pia imeelezwa kuwa kuna baadhi ya Shule madasa
hayana milango na nyingine katika Kata ya Goba hazina madarasa na hivyo kufanya
wanafunzi kusoma wakiwa chini ya Mwembe.
MIUNDOMBINU
Katika hali nyingine, Madiwani hao wameonyesha
kutokuwa kuwa imani na wakandarasi kutokana na barabara nyingi kujengwa chini
ya kiwango huku wakilipwa fedha zote za miradi.
Songoro Mnyonge anasema katika Kata yake kuna
Barabara inamiaka sita sasa ya urefu wa mita 800 hadi sasa haijakamilika huku
wananchi wakiwa hawajui kwa nini mkandarasi huyo hamali ujenzi wa barabara
hiyo.
Naye Kinyafu Diwani wa Saranga anasema kuna barabara
ya kilomita 7 inayounganisha kata ya Saranga na Kimara mkandarasi hajamaliza mpaka na ameitelekeza barabara
hiyo huku akiwa amelipwa fedha zote mil 400.
“Ninashindwa kuelewa mhandisi wa wilaya aliyemleta
mkandalasi Yule ana akili timamu au hajasoma, amemleta mkandarasi bila taarifa
kwenye Serikali ya Mtaa wala Ofisi ya Kata, sasa mkandalasi anapita
vichochoroni baada ya kuharibu” alisema Kinyafu.
AFYA
Katika sekta ya Afya, Halmashauri imesema
inajumlanya vituo vya Afya 25 huku vituo vinne vya Magomeni, Sinza,
Mwananyamara na Boko vikiwa na magari ya kubebea wagonjwa na imetenga fedha za
kugharimia wagonjwa akina mama katika vituovisivyo na magari na kusisitiza kuwa
wagonjwa hawatakiwi kulipa gharama hizo.
Aidha wamesema kuwa wanajiandaa kufanya upanuzi wa
vituo vilivyopo kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya
Mwanyamala.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni