HOSPITALI YA AGA KHAN YAISHAURI SERIKALI,NI KUHUSU WAUGUZI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
SERIKALI nchini imetakiwa kuongeza wahudumu wa afya
wakiwemo Wauguzi na Madaktari katika Hospitali zote nchini ili kuondokana na
tatizo la wauguzi kuwahudumu wagonjwa wengi kuriko idadi ambayo Wauguzi
wanatakiwa kuwahudumu.
Hayo yamesemwa na Lucy Hwai ambaye ni Mkurugenzi wa
Wauguzi katika Hospitali ya Aga Khan nchini,
wakati wa Maazimisho ya siku ya Wauguzi Dunia ambapo Hospitali hiyo nayo
iliadhimishwa siku hiyo,
Ambapo Amesema kwa sasa Fani ya Wauguzi nchini inakumbana
na Changamoto kubwa ikiwemo wauguzi kuwahudumia wagonjwa wengi kuriko idadi
inayotakiwa.
Amesema kwa mujibu wa shirika la Afya la Dunia
(WHO) linatoa mwongozo kwa wauguzi
kuwahudumu wagonjwa watano kila siku,lakini amedai kwa watanzania imekuwa
ikikwenda kinyume ambapo Muuguzi mmoja anasimamia wagonjwa zaidi ya 60 jambo
analodai linachangia kurudisha nyuma sekta ya afya.
Amesema kwa Sasa Serikali inatakiwa kuliwekea mkazo
suala la wauguzi ikiwemo kuwekea mazingira rafiki katika Hospitali zote nchini
hususani zilizopo Vijijini ili wauguzi hao wafanye kazi kwa umakini zaidi ili
kuondokana na tatizo la Vifo vinavyotokana na kusababishwa na mazingira mabovu
ya Wauguzi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni