BUNGE LAVURUGIKA TENA,UBABE BABE WA NAIBU SPIKA WACHANGIA,SOMA HAPO KUJUA
BUNGE la Tanzania limeahirishwa. Ni kutokana
na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kugomewa kuwasilisha
hoja binafsi kuhusu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kusimamishwa, anaandika Faki Sosi.
Hatua hiyo imetokana na Tulia Ackson, Naibu Spika kugomea mwongozo
uliotolewa na mbunge kutoka Ukawa kuhusu kujadiliwa taarifa ya kusimamishwa kwa
wanafunzo kutoka chuo hiko.
Taarifa kutoka
bungeni zinaeleza kwamba, Ackson aligomea taarifa hiyo jambo limezua mzozo na
hatimaye wabunge kuamua kutoka nje ikiwa ni ishara ya kutoridhika na uamuzi wa
kiti cha spika.Mwanahalisi Online linaendelea
kufuatilia.
Juzi Udom
kilitoa taarifa ya kusimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu
ya ualimu wa Sayansi, Hisabati na Teknolojia kwa ngazi ya Stashahada na kisha
kutaka waondoke chuoni hapo mara moja.
Tangazo hilo
liliwataka wanafunzi hao kuondoka kati ya juzi na jana saa 12 jioni. Tangazo
hilo lilieleza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo katika ufundishaji wa
stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao kurejea majumbani na kwamba wataelezwa
mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.
Kozi ya
Stashahada ya Ualimu wa Sayansi, ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Mstaafu,
Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la walimu wa sayansi na ilikuwa
inatolewa UDOM pekee.
Waliokuwa na
sifa za kujiunga na kupewa mikopo ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na
kufaulu vizuri masomo ya sayansi.
Wanafunzi hao
waliokuwa wamekopeshwa na serikali wamesimamishwa siku mbili baada ya wenzao
zaidi ya 480 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph kusimamishwa baada ya kubainika
kutokuwa na sifa za kudahiliwa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni