Zinazobamba

IDADI YA MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YAONGEZEKA,MUSUSA ATAJA CHANZO,SOMA KUJUA




Pichani ni Meneja Mauzo na Biashara wa (DSE),Patrick Mususa akizungumza na Waandishi wa habari(Hawapo pichani)kuhusu hali ya mauzo katika soko hilo
NA KAROLI VINSENT
MAUZO ya  Soko la Hisa Mkoani Dar es Salaam (DSE) kwa wiki hii yameongezeka kwa asilimia 76 kutoka sh.bilion 2.8 kwa wiki iliyopita hadi kufikia sh. bilioni  4.9 kwa hiki hii,
Huku pia Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa wiki hii zimeshuka kwa asilimia 20,Milioni 2.2 kutoka Milioni 2.8.

Akizungumza Dar es Salaam leo Meneja mauzo na Biashara wa (DSE), Patrick Mususa amesema kuongezeka kwa mauzo katika soko hilo kumechangiwa na idadi kubwa ya wafanya biashara kujitokeza kununua hisa hizo

Hata hivyo,Mususa ameyataja  makampuni yaliyoongoza katika wiki ni  pamoja na Benki NMB kwa asilimia 47.85,  CRDB  asilimia 38.34 na kampuni ya Swissport  asilimia 10.00.

Mususa pia ametaja ukubwa wa mtaji wa soko umeongezeka asilimia 0.5 kutoka Trilioni 22.0 hadi Trilioni 22.1 ambapo ukubwa  mtaji wa makampuni ya ndani umepungua kwa asilimia 0.1 kutoka Trilioni 8.5 hadi kufikia  Trilioni 8.4

Aidha Mususa amesema  Sekta ya viwanda (IA)  imepungua kwa pointi 2.72 ambapo  huduma za kibenki na kifedha
(BI) zimeshuka kwa pointi 10.36 baada ya bei kushuka kwenye kaunta za CRDB  kwa asilimia 1.33 wakati  huduma za kibiashara (CS) nazo zimeshuka kwa pointi 16.75 baada ya bei kushuka kwenye kaunta ya SWISSPORT 0.59.

Hakuna maoni