Zinazobamba

*UGENI KUTOKA AFISI YA RAIS ZANZIBAR WAKAMILISHA ZIARA MAALUMU KWA KUTEMBELEA MIRADI MBALIMBALI JIJINI DODOMA*


Ugeni kutoka Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji kupitia Taasisi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Zanzibar leo tarehe 06/02/2025 wametembelea Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo "SIDO"  pamoja na  Soko Kuu la Machinga Jijini Dodoma.Lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuona namna huduma zinavyotolewa kupitia maeneo hayo na jinsi zinavyowanufaisha  mwananchi wa kawaida.Ziara hiyo imeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi ndugu Condrad Millinga.


Hakuna maoni