HATIMAYE AZAM FC YAZINDUA DUKA LAKE LA VIFAA VYA MICHEZO, YANGA ,SIMBA BADO ZIPOZIPO SANA
Mkurugenzi mtendaji Wa Timu ya Azam FC Saad Kaawembaakiwa katika uzinduzi wa Duka jipya la vifaa vya michezo la Azam |
Klabu ya Soka ya Azam Fc imefanikiwa kuweka historia ya kipeke baada ya kufanikiwa kufungua duka la vifaa vya michezo la timu hiyo jambo ambalo kwa muda mrefu vilabu vikongwe vya Simba na Yanga vimeshindwa kulitekeleza.
Duka hilo lililopo Karibu na Mtaa wa Swahili na Mkunguni Mjini Kariakoo limesheni jezi zenye nembo ya Azam Fc na kwamba lina aina zote za jezi zikiwamo za watoto na wakubwa.
Akifungua duka hilo,Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo Saadi Kawemba amesema ni matumaini yao kuwa duka hilo litakidhi mahitaji ya mashabiki wa Klabu hiyo ambao kwa muda mrefu walikuwa wanatafuta sehemu ya kupata Jezi.
Amesema wameamua kufungua duka hilo karibu na makazi ya watu ili kuwapa fursa ya kufikia huduma hizo kwa urahisi na hivvyo kuweza kununua jezi hizo.
Akizungumzia kuhusu suala zima la bei, Kawemba amesema mashabiki wa timu hiyo na wale wasio mashabiki wasiogope kufika dukani hapo na kuuliza jezi hizo kwani wamepanga bei ambayo inawezekana.(Affordable price)
"Kama unavyoona tumeweka karibu an standi hii ya masaki hapa Kariakoo lengo letu si madereva ndio wanunue pekee lakini na wale abiria watakuwa miongoni mwa wateja wetu...bei zinawezekana kabisa" Alisema
Aidha akizungumzia kuhusu watu wanaohitaji kuwa mawakala wa Jezi za Azam, Kawemba amesema, Milango iko wazi waje wazungumze na kuona ni jinsi gani wanaweza kuwahudumia.
Amesema Duka litakuwa wazi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na mbili na nusu jioni hivyo ni fursa kwa watu kutembelea duka hilo.
"Tutakuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumbi na mbili lakini tutafanya utaratibu ili tuone jinsi tutakavyofanya kazi hadi usiku, ili tuweze kuwahudumia wale wanaotoka makazini" Alisema.
Duka hilo ni kama limekuja kujibu mahitaji ya mashabiki wa mpira hapa nchini ambao mara nyingi wamekuwa wakiuziwa jezi mitaani bila kujua ubora wa jezi zenyewe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni