Zinazobamba

MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YAPUNGUA,MUSUSA ATAJA CHANZO CHAKE,SOMA HAPO KUJUA

Pichani ni Meneja Mauzo na Biashara wa (DSE)

Patrick Mususa (picha na Maktba)





MAUZO katika Soko la Hisa Mkoani Dar es Salaam, (DSE) yameshuka kwa asilimia 59 kutoka sh.bilioni 6.84 kwa wiki iliyopita  hadi kufikia shilingi Bilion 2.8 kwa wiki hii.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo,

Hata hivyo, Idadi ya hiyo ya hisa zilizouzwa na kununuliwa  zimeshuka kwa asilimia 26 kutoka milioni 3.8 hadi kufikia Milioni 2.8.

 Patrick Mususa ambaye ni Meneja Mauzo na Biashara wa (DSE) Amewaambia waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,kuwa kiwango hicho cha mauzo kimeshuka  katika soko hilo kumechangiwa na kupungua ukubwa wa Sekta ya huduma za kibeki na kifedha kwa pointi 7.87.

Mususa pia amezitaja  kampuni zilizoongoza kwa mauzo katika soko hilo ni pamoja na  Benki ya CRDB kwa Asilimia 92.40, ikifwatiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa asilimia 4.16 na Benki ya maendeleoya wakulima (MBP) kwa asilimia 1.61.
Mususa amesema ukubwa wa mtaji wa Soko umebaki kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 22 ambapo wa mtaji wa makampuni ya ndani umeongezeka kwa asilimia 1 hadi kutoka Trilioni 8.4 hadi kufikia Trilioni 8.4.

Aidha Mususa amebainisha kuwa  Viashiria katika Sekta ya viwanda vimeongezeka kwa pointi 36.26 baada ya bei za hisa za TOL na TBL kupanda kwa asilimia 3.75 na 1.14 ambapo sekta ya huduma za kibiashara  zimebaki kwenye kiwango kile kile cha sh. 3,697.92.

Sanjari na hayo,pia Mususa amesema jumla ya wanafunzi Vyuo Vikuu waliojiunga katika shindano la (Scholar Investment Challenge 2016) linalo endeshwa na taasisi hiyo wamefikia 3,160 kutoka katika vyuo mbalimbali nchini.


Mususa amefafanuwa

kuwa  mwanafunzi aliyekuwa anaongoza katika shindano hilo wiki iliyopita alifikia mtaji wa sh.1,117,585, ambapo  mtaji wake umeshuka hadi kufikia sh. 1,112,135.

Hakuna maoni