UKAWA WAPAMBANA NA MAJANGILI WA TEMBO BUNGENI,WASHIKA PABAYA SERIKALI YA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
Tembo aliyeuwawa na majangili |
OPERESHENI Tokomeza Ujangili
iliyofanyika tarehe 4 Oktoba 2013 haijafika kikomo. Vyama Vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) leo bungeni vimedai idadi ya majangili waliokamatwa, anaandika Faki Sosi.
Ni kwa kuwa, mpaka sasa wameeleza kutoona matokeo ama utekelezwaji
wa maazimio ya bunge yaliyofikiwa kutokana na operesheni hiyo.
Ni operesheni
ilisababisha Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wake wanne
kufuatia wabunge kuungana bila kujali itikadi za vyama vyao kupinga unyanyasaji
uliofanywa wakati huo.
Mawaziri
walioondolewa walikuwa David Mathayo (Mifugo), Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya
Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na
Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) ambaye alijiuzulu.
Esther Matiko,
Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni katika Wizara ya Maliasili na
Utalii wakati akiwasilisha maoni ya upinzani kuhusu Mapato na Matumizi kwa
Mwaka wa Fedha 2016/17 leo amesema;
“Ni muda mwafaka
sasa Kambi Rasmi kutaka kuelewa ni majangili wangapi baada ya operesheni hiyo
kumalizika mali zao zimekamatwa na tayari kesi zao ziko mahakamani au tayari
wamefungwa?”
Esther amesema,
pamoja na operesheni hiyo kuwa na athari kubwa lakini watu wengi walioathirika
hawajalipwa fidia zao mpaka sasa.
Mefafanua kuwa,
kwa mujibu wa Taarifa ya Serikali, vitendo vya ujangili vinavyofanyika nchini
vimegawanyika katika makundi mawili
Kundi la kwanza
ni Ujangili wa Kujikimu; na kwamba aina hii inahusisha watu wenye kipato kidogo
na hulenga zaidi katika kujipatia kitoweo na fedha kwa ajili ya kukidhi
mahitaji mengine.
Aina ya pili ni
Ujangili wa Biashara; Aina hii ya ujangili inahusisha zaidi watu wenye uwezo
mkubwa wa kifedha na hulenga kupata nyara zenye thamani kubwa.
“Wanyama
wanaoathiriwa zaidi na aina hii ya ujangili ni pamoja na Tembo, Faru, Simba na
Chui,” amesema.
Amesema “…tarehe
04 Oktoba 2013 ilizindua Operation Maalum ya kupambana na ujangili huo ili
kuzuia vitendo hivyo ndani na nje ya hifadhi za Taifa, katika Mapori ya Akiba,
Mapori Tengefu.
“Pia kuwatambua
mapema majangili na kujua nyendo zao ndani na nje ya maeneo ya hifadhi kwa
kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wahusika wakuu wa nyara hizo
za Taifa.”
Amesema, Rais
Jakaya Kikwete aliunda tume maalum iliyoongozwa na Mhe Jaji Msumi ya
kushughulikia suala hilo, lakini taarifa ya tume hiyo hadi sasa imeishia kwenye
makabati ya Ikulu na Watanzania hawakupata nafsi ya kuelewa nini Jaji Msumi
aliona na kushauri.
“Aidha hakuna
hatua zozote za fidia zimechukuliwa kwa waathirika wa operation hiyo ambao
wengi walipoteza mifugo yao, walichomewa nyumba zao, walibakwa, walidhalilishwa
na wengine walipoteza ndugu na jamaa zao na wengine wamekuwa walemavu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni