WAZIRI WA UJENZI AIAGIZA MAMLAKA YA HALI YA HEWA KUTEKELEZA HAYA, ASEMA WASIPOWAJIBIKA YATAWAFIKA YA TPA
Waziri wa Ujenz, uchukuzi na Mawasiliano Prof
Makame Mbarawa ameiagiza mamlaka ya hali ya hewa hapa nchini (TMA) kuanza zoezi
la kuweka utaratibu wa kupimana kuhusu utendaji kazi katika kila idara ili
kuifanya mamlaka hiyo kuongeza ufanisi wake.
Akizungumza
na wafanyakazi wa taasisi hiyo, mara baada ya kutembelea idara mbalimbali ya mamlaka
hiyo,Prof. Mbarawa amesema kuna haja ya Mamlaka hiyo kuanza utaratibu wa
kupimana
Alisema
kufanya hivyo kutaongeza uwazi katika majukumu yao, kutawasaidia wafanyakazi
kupandishwa madaraja na pia kutakuwa hakuna minong’ono ya upendeleo katika
suala zima la kupandisha vyeo wafanyakazi.
“Naamini
mamlaka hii inawanasayansi na wanafanya kazi zao vizuri, lakini nataka mjue
sasa katika utawala huu mpya tunataraji kuanza kuweka utaratibu wa namna ya
kutimiza malengo ya kutoa taarifa muhimu za kitabiri, mimi nitamuakiza
mwenyekiti kutimiza hilo”
Katika
hatua nyingine Prof Mbarawa ameitaka taasisi hiyo kuanza kuipa kipaumbele
matumizi ya kidigitari na kuachana kabisa na matumizi ya makaratasi kwani sasa
dunia inapoelekea inakimbilia katika kuachana na matumizi ya makaratasi na hivyo
kupunguza gharama kwa serikali.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Waziri huyo kupita katika idara moja na kukuta taarifa
nyingi zikihifadhiwa kwa mfumo wa mafaili, jambo ambalo amesema si sahihi na
kuwataka wabadilike.
“Wakati
napita kukagua ofisi yenu nimefika sehemu moja nimeona matumizi ya makaratasi
ni makubwa, si vibaya lakini sasa tunapaswa kubadilika, tunauwezo wa kutunza
taarifa hizo kidigitari, nitazungumza na watu wa Mamlaka ya mawasiliano
Tanzania (TCRA) wawape mafunzo”Alisema
AKAGUA
MRADI WA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCO
Katika
hatua nyingine Waziri huyo amekagua mradi wa upanuzi wa barabara ya
Mwenge hadi Morocco yenye kilomita 4.3 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa
asilimia 95.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa ukaguzi huo Prof.Mbarawa
ameeleza kuwa tayari njia tano zimeanza kutumika kuanzia eneo la Mwenge hadi
Kijitonyama zenye urefu wa kilomita 2 huku kilomita nyingine 2.3 zikiwa katika
harakati za mwisho za kukamilishwa.
“Serikali
imedhamiria katika kuhakikisha kuwa inatatua kero ya msongamano wa
magari kwa kufanya upanuzi wa njia muhimu ili kurahisisha hali ya usafiri
jijini Dar es Salaam ” alisema Prof.Mbarawa.
Aliongeza
kwa kusema hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John
Pombe Magufuli alizindua mradi wa daraja la Kigamboni linalounganisha kurasini
na Kigamboni pamoja na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa
mradi wa flyover katika eneo la Tazara .
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)
Mhandisi.Patrick Mfugale ameeleza kuwa mradi huo umekabiliana na
changamoto mbalimbali ikiwemo uhamishaji wa mabomba ya maji safi na maji taka
katika eneo la Makumbusho na Mwenge ili kuendelea na ujenzi.
Novemba
30 mwaka jana Rais John Magufuli aliagiza kiasi cha shilingi bilioni nne
kilichopangwa kutumika katika shamrashamra za siku ya Uhuru kitumike katika
kazi ya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye
urefu wa kilometa 4.3 ili kuiunganisha barabara hiyo na ile ya Mwenge – Tegeta
yenye urefu wa KM 12 .
Hakuna maoni
Chapisha Maoni