Zinazobamba

WAMACHINGA UBUNGO WATAKIWA KUHAMA....MSAKO MKALI KUANZA KESHO




Operesheni kali inatarajiwa kuanza kesho katika eneo la ubungo ambapo wafanyabiashara mbalimbali wanatarajiwa kukamatwa kama wakikaidi agizo la meya wa manispaa hiyo Bw, Boniface Jacob aliyewataka wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga) kuacha kuuza biashara zao kando ya barabara.

Akizungumza na wafanyabiashara hao katika soko la Sinza Mawasiliano, Jacob amesema wamefikia hatua hiyo ili kuwafanya wafanyabiashara hao kuwa na vikazi maalum.

Amesema wameanza kwa kuwapa namba maalum ambayo ndio kielelzo chao cha kumiliki eneo la kufanya biashara eneo la Sinza.

"Tunawataka wafanyabiashara hawa kuhamishia biashara zao katika soko la Mawasiliano ambalo limetengwa maalumu kwa ajili ya biashara."


“Nawasihi wafanyabiashara wa Ubungo kuhamishia biashara zao katika eneo la soko la Mawasiliano tulilowatengea”.







Hakuna maoni