MEYA WA UKAWA KINONDONI AZIDI LETA NEEMA KINONDONI,SASA AWANEMESHA WAFANYABIASHARA,SOMA HAPO KUJUA
Boniface Jacob, Meya wa Halmashauri ya Kinondoni |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imewapa
wafanyabiashara wapatao 100 eneo la kufanyia biashara zao katika Soko la
Mawasiliano (Sinza), anaandika Happiness Lidwino.
Kwenye soko hilo,
wafanyabiashara hao hawatalipa ushuri kwa mwezi mmoja na kisha watatakiwa
kulipa.
Boniphace
Jacob, Meya wa Manispaa hiyo leo amesema, awali alifanya ziara katika maeneo
hayo na kuzungumza na wafanyabiashara ambapo aliwataka kutofanya biashara zao
kwenye eneo la Ubungo na badala yake kuhamia Mawasiliano.
“Soko
hili ni kwa ajili yenu nyie wamachinga, mama lishe kila mwenye biashara
aangalie kunakomfaa na kufanya biashara, kila mtu atapewa kitambulisho kutoka
manispaa kimtambulishe eneo lake husika,”amesema.
Amesema,
aliona si busara kuwaondoa wafanyabiashara hao bila kuwa na maeneo ya kwenda
kufanya biashara zao.
“Niliomba
wiki mbili kamati ya ulinzi na usalama ya kinondoni msivunjiwe hadi hapo
nitakapowatafutia eneo la kufanya biashara zenu, ni jukumu langu kujua
mtakwenda wapi. Kuanzia leo, atakayekuwa Ubungo asinisumbue, watu wangu wako
salama mawasiliano,” amesema.
Na
kwamba, hatarajii kuona Jeshi la Polisi au mgambo wanawasumbua wafanyabiashara
hao huku akiwaomba kuacha njia kwa wanunuzi watakaofika sokoni hapo.
“Hakuna
atakayekosa eneo la kufanyia biashara hapa, kila mtu atapata wauza mabegi ule
uzio upendeze kwa kutundika mabegi na wauza nguo pia, lakini pia msilipe ushuru
kwa mwezi mmoja baada ya mwezi mmoja ndiyo mtalipa,” amesema.
Meya
huyo amesema, wafanyabiashara ambao tayari wamepanga biashara zao
wasibugudhiwe, waliopewa na kutofanya biashara wapewe watu wengine wafanye.
Baadhi
ya wafanyabiashara waliokuwa wakiwahi nafasi katika eneo hilo, walilalamika kwa
wengine kutopata kwani tayari eneo limeonekana kuwa dogo.
Husna
Khamis na Amida Juma ni miongoni mwa wafanyabiashara ambao wamesema, wana
wasiwasi na maeneo hayo kutopata kwani waliowahi maeneo hayo asilimia kubwa si
wafanyabiashara waliopaswa kuondoka Ubungo.
“Mimi
sijapata eneo unavyoniona hapa, kila ninapoangalia naona majani watu wamewahi,
ingawa Meya ametuambia tuweke biashara kama eneo halina mtu, ukienda ndani
wanakuambi ulipe sh 140,000 ndiyo upate,” amesema Juma.
Awali
Jacob alisema, maeneo hayo yamegaiwa bure huku akisisitiza mtu atakayeuza atachukuliwa
hatua pamoja na kunyang’anywa eneo husika na kupewa mtu mwingine.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni