WAFANYABIASHARA SOKO LA NDIZI MABIBO SASA WAMVAA MEYA WA KINONDONI,
Soko
la ndizi mabibo limekuwa ni maarufu sana katika jiji la Daresalaam, wengi
wanalifahamu kutokana na umaarufu wake wa kuweza kurisha wakazi wa jiji la
Daresalaam bidhaa ya ndizi kwa manispaa zote za Jiji .
Ni
soko ambalo ndizi zote kutoka mikoa mbalimbali ya nchi ya Tanzania zinapokelewa
hapo na kusambazwa katika masoko mengine ya Jiji .
Masoko
ya Buguruni, Tandale, Ilala, Mwananyamala,sterio kule Temeke yamekuwa yakipokea
bidhaa ya ndizi kutoka soko hilo la Ndizi Mabibo.
Soko
hilo linahistoria ndefu, toka enzi hizo likiitwa soko la urafiki na baadae
wafanyabiashara kuhamia eneo jipya ya Mahakama ya ndizi.
Kutokana
na umuhimu wake,wakazi wa Jiji hilo wamekuwa wakifurika usiku na mchana
kujipatia bidhaa ya ndizi tayari kwa matumizi mbalimbali.
Fullhabari
ilipata fursa ya kuzungunmza na wafanyabiashara wa soko hilo kufuatia tetesi
zilizopo kuwa soko hilo kwa sasa wafanyabiashara wake wamekuwa wakifanya
biashara kwa hofu.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, mmoja wa wafanyabiashara hao Bw. Amosi Pengo amesema
kwa muda mrefu wamekuwa wakitoa kilio chao kwa viongozi wakuu wa halmashauri
lakini hakuna majibu ya kuridhisha dhidi ya wasiwasi wao.
Mjasiliamali akihesabu mapato yake |
Amesema
kilio chao kikubwa ni kutaka kurasimisha soko hilo kuwa soko kamili na hivyo
kodi inayotolewa na wananchi wa soko hilo iweze kuingia moja kwa moja katika
serikali,
Akizungumzia
athari wanayopata kutokana na soko hilo kutorasimisha kamili, Amesema wamekuwa
hawana uhuru wa kufanya biashara zao kwa hofu kuwa muda wowote soko hilo
linaweza kufutwa.
Amesema
licha ya soko hilo kukusanya mamilioni ya shilingi kwa njia ya kodi wanazotozwa
kila mwezi, hawaoni manufaa yake kwani hakuna huduma stahili zinazotolewa
Amesema inawezekana kabisa fedha hizo
zinaingia mifuko ya watu wachache na kushauri serikali kuangalia suala hilo.
“Tunadhani
Dar es salaam ya Makonda inahimiza usafi, lakini hebu angalia soko hili
limekuwa chafu kiasi ambacho wateja wamekuwa wakiteseka kupata huduma,
tunashangaa kwanini haya yote yanatokea wakati kodi inalipwa” alihoji Mapengohali.
Akizungumzia
hofu ya wafanyabiashara wa soko hilo, Amosi amesema watu katika soko hilo
hawana Amani kabisa na kuendelea kufanya biashara hapo badala yake wamekuwa
wakiishi kwa matumaini.
Katika
hatua nyingine wafanyabiashara hao wamemuomba Meya wa manispaa ya Kinondoni Bw Boniface
Jacob kuingilia kati na kulifanya soko hilo kuwa mikononi mwa serikali badala
ya kuendelea kumilikiwa na kiwanda cha urafiki.
“Sisi
Wafanyabiashara wa soko la ndizi mabibo urafiki jijini Dar es salaam tunaiomba
serikali kuharakisha ombi letu la muda mrefu la kubadili eneo hili la soko
kutoka kwenye kuendelea kuwa eneo la viwanda na kuwa eneo la soko rasmi ili
tuweze kufanya biashara zetu kwa uhakika ikiwa ni pamoja na kukopesheka na
kufadhiliwa” walisema
Kama unavyoona hapa ndipo Ndizi kutoka kila mkoa wa Tanzania
hushwa kwa ajili ya kusambazwa kila pembe ya Dar es lakini tumekuwa hatuthaminiwi kutokana na soko
kumilikiwa na kiwanda.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni