SERIKALI YA MAGUFULI YAIOGOPA FAMILIYA YA KIKWETE,NI KUHUSU SHIRIKA LA UDA,YAIBUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA
Mama Salma Kikwete (kulia) akicheza muziki na mwanaye, Ridhiwam Kikwete walipokuwa kwenye kampeni za Ubunge Chalinze |
SERIKALI imetetea uuzwaji wa hisa za Shirika la
Usafirishaji nchini (UDA) kwa Kampuni ya Simon Group na kwamba, kampuni hiyo
inamilika hisa hizo kihalali, anaandika Regina Mkonde.
Lawrance Mafuru, Msajiri wa
Hazina akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema,
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliiuzia UDA hisa kihalali.
Utetezi
huo unawapa pumzi Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na Ridhwan
Kikwete, mtoto wa rais huyo na Prof. Juma Kapuya, aliyekuwa Mbunge wa Urambo
Magharibi ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa wana hisa kwenye kampuni hiyo.
“Bodi
ya UDA iliyokuwepo muda ule ilikiuka taratibu za uuzaji wa hisa za serikali
bila ya Baraza la Mawaziri ambalo lenye mamlaka ya kufanya maamuzi ya uuzwaji
wa hisa kuamua kuuza hisa hizo,” amesema Mafuru.
Anaeleza
kuwa, Bodi ya UDA iliamua kuuza hisa kwa Kampuni ya Simon Group baada ya kuona
shirika hilo linayumba hivyo lilihitaji muwekezaji ili kulifufua.
“Baraza
la Mawaziri chini ya mwenyekiti wake ambaye ni rais halikukaa kikao cha kufanya
maamuzi ya kuuza hisa na kwamba, baada ya bodi kuona serikali inachelewa kutoa
maamuzi ikaamua kuuza hisa za serikali,” anasema.
Amefafanua
kuwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ndilo lililouza hisa zake kupitia
Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji hilo kwa kushirikiana na wajumbe wenzake
watatu akiwemo Mwanasheria wa Jiji.
“Kwa
mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na jiji, lilipokea fedha kutoka Kampuni ya
SGL kwa ajili ya manunuzi ya hisa zake na kwamba kwa sasa jiji halimiliki UDA,
” amesema.
Amedai,
UDA linamilikiwa kihalali na Kampuni ya SGL ambayo inahisa asilimia 51
iliyouzwa na jiji pamoja na serikali ambayo ina hisa ya asilimia 49.
“Aliyeuza
hisa za UDA kwa SGL ni Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam
kwa kushirikiana na wajumbe wengine watatu akiwemo Mwanasheria wa Jiji, sasa
kama Masaburi hakuwa Meya halali wa jiji basi hisa hazikuuzwa kwa kampuni ya
SGL,” ameeleza.
Akieleza
mwanzo wa ugawaji wa hisa za UDA kutoka kwa serikali kwenda Halmashauri ya Jiji
la Dar es Salaam ambapo amesema, serikali iliona bora igawe hisa za asilimia 51
kwa jiji hilo ambalo UDA linapofanya kazi zake.
“Mnamo
mwaka 1974 serikali ilianzisha shirika la UDA, mwaka mmoja baadaye serikali
iliamua kugawa hisa ya asilimia 51 kwenda kwa jiji la Dar es Salaam na yenyewe
kubaki na asilimia 49 ambazo inazo hadi sasa,” amesema.
Hivi
karibuni Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Baraza la Halmashauri ya
Jiji hilo lilikana kuitambua Kampuni ya SGL kuwa, mmiliki halali wa UDA.
Kwa
mujibu wa maelezo yao, Masaburi alichukua jukumu la kuuza hisa za jiji kwa
Kampuni ya SGL bila kulishirikisha baraza la madiwani la kipindi ambacho uuzaji
ulipofanyika.
Siku
tatu zilizopita, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo alisema, halmashauri
haikuuza UDA licha ya Simon Group Limited kudai kununua.
Kwenye
mkutano huo ambao pia uliohudhuriwa na Isaya Mwita Charles, Meya wa Jiji la Dar
es Salaam Kubenea alisema, mkutano uliokabidha UDA kwa Simon Group uliitishwa
bila baraka za wenye mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na
kwamba, ulihudhuriwa na watu wanne tu.
“Kwanza
tunataka mtambue halmashauri haikuuza UDA kwa kuwa, Simon Group Limited
wametumia hati ya UDA – mali ya wananchi kufanya biashara. Haturudishi fedha
hizi mpaka tufanye hesabu, tujue kampuni hii imepata faida kiasi gani.
“Hata
katika mradi wenyewe wa UDA-TR, kumesheheni utapeli. Unaoitwa mkutano mkuu
maalum wa wana-hisa wa tarehe 10 Juni 2011, uliosimamiwa na Didas Masaburi,
aliyekuwa Meya wa Jiji kuidhinisha pamoja na mengine, uuzaji wa hisa za UDA,
haukuwa halali,” amesema Kubenea.
Kubenea
amesema, mkutano uliokabidha UDA kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za
wenye mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na kwamba,
ulihudhuriwa na watu wanne tu
“Watu
hawa ni Dk. Didas Masaburi mwenyewe ambaye alikuwa mwenyekiti; Mkurugenzi wa
Simon Group, Robert Kisena ambaye alikuwa katibu; Mwanasheria wa jiji, Isaac
Nassor Tasinga na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Phillip Mwakyusa,” amesema Kubenea
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni