Mapenzi yaondoa uhai wa mwanafunzi
MWANAFUNZI
wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Elimu (Duce), jijini Dar es Salaam,
Bertha Mwarabu (23), ameuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kuchomwa kisu kwenye
titi na tumboni kwa kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, tukio hilo
lilitokea usiku wa kuamkia jana katika hosteli za chuo hicho zilizopo Mabibo,
jijini Dar es Salaam.
Kamanda
Kalunguyeye amemtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Masamba Musiba (27)
ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho, ambacho ni sehemu
ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Amesema
mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:45 usiku baada ya Musiba kuingia chumbani kwa
marehemu ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake na kuanza kumshambulia kwa kisu.
Ameongeza
kuwa baada ya marehemu kuanza kushambuliwa, alipiga kelele kuomba msaada na
ndipo wanafunzi wenzake walipokwenda na kumkamata mtuhumiwa wakati akijaribu
kukimbia.
Amesema
kelele za marehemu, ndizo zilizowashtua wanafunzi wenzake.
Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa marehemu alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu lakini alifia njiani.
Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa marehemu alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu lakini alifia njiani.
Mtuhumiwa
anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa
katika Hospitali ya Mwananyamala.
Kwa
upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza
Mukandala, amesema tukio la mauaji hayo ni la kwanza kutokea chuoni hapo.
Profesa
Mukandala alisema tangu aanze kufanya kazi chuoni hapo kwa miaka mingi,
hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo na kuongeza kuwa amesikitika kwa
kuondokewa na mwananfunzi huyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni