Zinazobamba

MAMBO YANAZIDI KUWA MAZURI KWA UKAWA,SASA WAPATA NAIBU MEYA JIJI LA DAR,SOMA HAPO KUJU

Pichani ni anayeapishwa ni Mussa Swedi Kafana Diwani wa Kata ya Kiwalani ambaye ni Naibu Meya Mteule wa jiji
Anae muapisha ni Aziza Kalli Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Sokoine Drive.





HATIMAYE uchuguzi wa  Naibu meya wa Jiji la Dar es Salaam ambao ulikuwa unasubiriwa umemalizika na Mussa Kafana ametengazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo

Kafana  ambaye ni Diwani wa Kata ya Kiwalani jijini hapa kupitia Chama cha Wananchi (CUF) ameibuka kuwa mshindi kwa kupata kura 10  akimshinda mpinzani wake kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM),Mariam Lurida ambaye alipata kura 6,

Uchaguzi huo ambao umefanyika leo mapema unakuwa umekamlisha chaguzi zote za nafasi za umeya ambazo zilikuwa zinahairishwa mara kwa mara.

Akizunguma mara baada ya kutawazwa kuwa Naibu meya,Kafana amewataka Madiwani wote wa jiji na wabunge kuondoa itikadi zao za chama kwa kujiingiza katika mipango ya kuwatumikia wananchi.
Khafani ambaye anaungwa mkono na Vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) amesema kwa sasa Wakazi wa Dar es Salaam wategemee kasi ya maendeleo ambayo

ameifananisha kasi hiyo na Kasi aliyokuwa nayo Rais Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,John Magufuli katika kuwatumikia wananchi.
Kwa upande wake Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea ambaye naye ni mjumbe katika Baraza la Madiwani ammetaka Meya huyo kuhakikisha anakuwa katika mstari mbele kuondoa mikataba yote anayodai ni  ya kifisadi.
Kubenea ameitaja mikataba hiyo ni mikataba ya Machinga Complex,tozo za kupaki magari.

Hakuna maoni