CHADEMA YALIA NA RAIS MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
Benard Mwakyembe, Kaimu Mwenyekiti wa Dar es Salaam kubwa(Great Dar es Salaam)ya Chadema |
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kimemtaka Rais John Magufuli kutumbua majipu makubwa yaliyokuwepo ndani ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kufuata taratibu za uongozi kwenye utumbuaji huo,anaandika Faki Sosi.
Benard Mwakyembe, Kaimu
Mwenyekiti wa Dar es Salaam kubwa(Great Dar es Salaam)ya Chadema amesema kuwa
utumbuaji wa majipu mbele ya umma ni kinyume na taratibu za uongozi akitaja
mfano wa kusimamishwa kazi hazalani kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson
Kabwe sio utaratibu nzuri kwani angiitwa na kuchuunguzwa
“Ingawa
ni vema kuwawajibisha viongozi wazembe lakini Rais anafanya maamuzi kwa mzuka
wa ushabiki wa watu pasi nakufuta taratibu za uongozi”amesema Mwakyembe.
Mwakyembe
amesema kuwa nyuma ya pazia la utumbuaji majipu kuna majipu makubwa ambapo
utaratibu wa kuhojiwa kwa waliotumbuliwa utafanya kupatikana kwa mizizi ya
majipu hayo.
“Nyuma
ya Wilson Kabwe kuna Mstahiki Meya aliyemaliza Muda wake ambaye ni Didas
Masaburi naye alipaswa kuwajibishwa kama mtuhumiwa kutokana na kuwa yeye ni mtu
wa pili kusaini mikataba yote ya Jiji .
Na
madiwani wote aliohusika na viongizi wote wa serikali wawajibishwe” amesema
Mwakyembe.
Aidha alisema kuwa wamesikitishwa na
kitendo cha Magufuli kutumia kumbagua Meya wa Jiji la katika ufunguzi wa daraja
la Julius Nyerere maarufu kama daraja la Kigamboni baada ya kumfanya awe kama
mvamizi kwenye uzinduzi huo.
Henri
Kileo Katibu Mkuu Dar es Salaam Kubwa amesma kuwa Mkuu wa Mkoa ni kinara wa
vitendo vya ubaguzi wa viongozi wa upinzani ili kuwadhoofisha .
Kadhia
hiyo ya ubaguzi imehusishwa pia kwa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC)
kutorusha matangazo au habari inayowahusu wapinzani.
Katibu
Mkuu wa Great Dar es Salaam, alisema siku ya uzinduzi wa daraja hilo Mstahiki
Meya alipokuwa anahutubia baada ya kupewa nafasi TBC walizima matangazo.
Mwakyembe
anasema kuwa kwa shirika hilo kutorusha matangazo ya vyama vya upinzani sio
mara ya kwanza kwani wao hawarushi matangazo ya aina yoyote yale
yanayowalenga wapinzani
“ikiwa
ile ni chombo cha habari cha taifa kinochoendeshwa kwa kodi za wananchi
lakini wanahubiri ubaguzi ikiwa na vyama navyo ni vya walipa kodi
vilivyosajiliwa kwa mujibu wa katiba.
Kama
wanataka iwe hivyo basi waifanye TBC iwe kama Radio Uhuru ya CCM wananchi wajue
kwamba ni shirika la utangazaji la CCM” amesema Mwakyembe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni