CUF WACHACHAMAA NA SERIKALI YA RAIS MAGUFULI,WAIBUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama cha Wananchi (CUF) Abdul Kambaya akizunguma na Waandishi wa Habari leo Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho yaliopo Jijini Dar es Salaam, |
NA KAROLI VINSENT
WAKATI ikiwa Vyombo ya Habari vya binafsi pamoja na
Serikali kuzuiliwa kuonesha mikutano ya
Bunge la jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Live (moja kwa moja,)
Wadau mbali mbali wamendelea kukosoa hatua hiyo kwa
kusema serikali yeyote ya hovyo na isiyojihamini ndio inataka Bunge hilo
kutorushwa moja kwa moja kwa kile kinachoitwa ni kitendo cha serikali kuficha matendo ya maovu
yasijulikane kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa
Chama cha Wananchi (CUF) Abdul Kambaya, ambapo katika kikao Mkutano wake na
Waandishi wa Habari,makao mkuu ya Chama hicho leo jijini Dar es Salaam,amesema
kitendo cha serikali ya Rais John Magufuli kukataza Bunge lisionyeshwe ni wazi
kuwa serikali hiyo imeanza kuongoza nchi Kidikteta.
Amesema
Dalili za utawala wa Rais Magufuli za kubana uhuru wa habari zilianza mapema
pale ambapo Waziri wa Habari,utamaduni,sanaa na michezo,Nape Nnauye
alipolifungia Gazeti la Mawio na baadae Waziri huyo akazuia Bunge lisirushwe
Live (Moja kwa Moja),
“Ni wazi
Serikali hii umekuwa ni ya Kidiktea ambayo haitaki kuambiwa ukweli,na imeanza
kuvunja katiba ya nchi ambayo inataka Mwananchi kupata taarifa,lakini leo
serikali hii ya Magufuli imewazuia wananchi wasipate haki yao ya msingi ya
kuonyeshwa kwa bunge moja moja”amesema Kambaya.
Kambaya
ameeleza kuwa bunge likirushwa moja kwa moja linaongeza uwajibikaji, uwazi
hivyo kutolionesha moja kwa moja ni kinyume na sheria ya Uhuru wa Habari
kifungu cha 18 katiba ya mwaka 1977.
Naibu
Mkurugenzi huyo amesikitishwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuvinyima uhuru vyombo binafsi vya habari katika kuripoti habari za bunge kwani
ameseme kuwa Bunge limeanzisha kituo chake cha kurusha matangazo ambapo
wanahabari watakuwa wanapatiwa habari na chombo hicho, pia hairuhusiwi kwa
muandishi kuingia na kamera au kinasa sauti bungeni jambo ambalo amelifananisha
na udikteta.
Kutokana
na hayo yote Naibu Mkurugenzi wa Habari Kambaya amesema kuwa chama chake cha
CUF kipo tayari kushirikiana na vyombo vya habari binafsi kupambana kufanikisha
kuwa Uhuru wa vyombo vya habai unapatikana kwani sababu ya gharama za
uendeshaji sio sababu ya msingi kwani luninga ya Taifa inapata ruzuku ya
serikali inayotokana na kodi za wananchi, hivyo isiwe kisingizio cha kuwaficha
wananchi ili madudu ya serikali yapite bila kupingwa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni